October 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Simba kuwavaa Wabotswana klabu bigwa

Spread the love

 

TIMU ya soka ya Simba ya jijini Dar es Salaam nchini Tanzania, itacheza na Jwaneng Galaxy FC ya Botswana katika michuano ya klabu bigwa barani Africa. Anaripoti Damas Ndelema, Tudarco … (endelea).

Jwaneng imefika hatua hiyo baada ya kuitoa klabu ya Diplomates FC ya Afrika Kusini kwa ushindi wa jumla wa bao 2-1.

Timu hizo yaani Jwaneng na Simba zitakutana tarehe 15 Oktoba 2021 kwa Simba kuanzia ugenini na marudiano yatafanyika tarehe 22 Oktoba 2021,jijini Dar es Salaam katika dimba la Benjamin Mkapa.

Mshindi katika mchezo huo, atakata tiketi ya moja kwa moja kwenda makundi ya klabu bigwa na atakae poteza atakwenda kucheza mtuano ‘play off’ ili kufuzu makundi ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.

error: Content is protected !!