June 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Swahiba wa Dk. Salim afariki dunia

Rais wa zamani wa Algeria, Abdelaziz Bouteflika

Spread the love

 

RAIS wa zamani wa Algeria, Abdelaziz Bouteflika amehitimisha safari ya maisha yake hapa duniani akiwa na miaka 84. Anaripoti Victoria Mwakisimba, TUDARCo kwa msaada wa mitandao ya Kimataifa..(endelea).

Alikuwa swahiba mkubwa wa waziri mkuu wa Tanzania, Dk. Salim Ahmed Salim. Salim alikuwa waziri mkuu kati ya Aprili 1984 hadi 5 Novemba 1985, wakati wa utawala wa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Salima aliwahi kuwa katibu mkuu wauliokuwa Umoja wa nchi huru za Afrika OAU abayo sasa ni AU.

Bouteflika aliyehudumu nafasi ya urais kuanzia mwaka 1999 hadi 2019, alifikwa na mauti jana Ijumaa, tarehe 17 Septemba 2021.

Ni baada ya kuugua kwa muda mrefu ugonjwa wa kiharusi uliomfanya kupoteza uwezo wa kutembea na kuzungumza na mara ya mwisho kuonekana hadharani ilikuwa mwaka 2014.

Rais huyo ambaye alitolewa madarakani kwa shinikizo la jeshi na maandamano ya kiraia nchini humo, alianza harakati za kisiasa akiwa kijana mdogo.

Mwaka 1962 akiwa na miaka 25, aliweka historia nchini humo kuwa waziri mwenye umri mdogo wa vijana na michezo.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad (kulia), Dk. Salim Ahmed Salim – Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere (katikati) na Joseph Butiku – Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo wakiwa kwenye mkutano wa kujadili amani nchini

Aidha, akiwana miaka 26, Bouteflika aliweka rekodi ya dunia ambayo haijavunjwa mpaka sasa ya kuwa waziri mwenye umri mdogo wa mambo ya nje. Alishika wadhifa huo kwamiaka 16.

Baada ya kuachia madaraka, Bouteflika alikuwa akiishi kwenye nyumba yake huko zerlada magharibi mwa Algeria, hata hivyo taarifa ya kifo chake imeonekana kutotiliwa mkazo.

Katika kipindi cha uongozi wake wa waziri na rais wa Bunge la Umoja wa Mataifa, mwaka 1974, Bouteflika alimualika kiongozi wa Palestina wakati huo, Yasser Arafat kuhutubia jambo ambalo halikutarajiwa na wengine.

Kupitia hotuba hiyo, ilitoa mwelekeo chanya wa siasa za mashariki ya kati. Pia alisisitiza China inastahili kuwa na uwakilishi katika Umoja wa Mataifa huku akipinga ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini.

Bouteflika aliishi uhamishoni kati ya miaka ya 1980 akikimbia kufunguliwa mashtaka ya ufisadi ambayo baadaye yalifutwa.

Alirejea nchini mwake miaka ya 1990 na miaka tisa baadaye akawa kiongozi wa juu wa Algeria, akiwa Rais wa kwanza raia wa taifa hilo katika kipindi cha miaka 30 iliyopita.

Akiwa madarakani, alitafuta suluhu ya mapigano kati ya jeshi na wanamgambo waliojihami ambao walikuwa wakipigana katika vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo ambapo zaidi ya raia wa nchi hiyo, 150,000 waliuawa.

Mwaka 2008, Rais Bouteflika alianzisha mchakato wa kubadilisha katiba ya Algeria ambao uliondoa ukomo wa muhula miwili wa marais- na kuchaguliwa tena mara mbili licha ya kukabiliwa na mashtaka ya udanganyifu.

Wakati maandamano ya kupigania mageuzi ya uongozi katika nchi za kiarabu yalipozuka mwaka 2011 kaskazini mwa Afrika, Bouteflika aliongeza haraka ruzuku ya umma na kumaliza hali ya hatari nchini Algeria iliyodumu kwa muda mrefu.

error: Content is protected !!