Thursday , 30 March 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Shule za sekondari, msingi zatangaziwa fursa
Habari Mchanganyiko

Shule za sekondari, msingi zatangaziwa fursa

Spread the love

Mfuko wa Misitu Tanzania (TaFF), umetangaza kutoa ruzuku ya Sh.5 milioni kwa kila andiko la mradi inayohusiana moja kwa moja na upandaji miti katika shule za msingi na sekondari. Anaripoti Mwandishi Wetu, Arusha…(endelea).

Hayo yamesemwa na Juma Ally, Afisa Mradi wa TaFF, katika maonyesho ya nne ya Mifuko na Programu za Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi yanayoendelea jijini Arusha.

Amesema, lengo la maonyesho hayo ni kuwaelezaa wananchi jinsi wanavyoweza kupata fursa ya kuomba ruzuku kwenye miradi inayohusiana moja kwa moja na upandaji miti katika nyanda kame na miradi inayohusiana na uendelezaji wa sekta ndogo ya ufugaji nyuki.

”Mfuko wa Misitu Tanzania unatoa ruzuku ya kuanzia Sh.5 milioni hadi Sh.50 milioni, hivyo wadau wa misitu na nyuki wanaweza kupata fedha hizi iwapo watatuma maandiko ya kuomba ruzuku ya miradi,” amesema

”Kwa mujibu wa tangazo la TaFF la kuhitisha maandiko ya miradi kwa mwaka huu kipaumbele kimetolewa kwa shule za msingi na sekondari pamoja na taasisi zitakazowekeza katika miradi ya ujenzi wa vituo vya kuchakata mazao ya nyuki na misitu,” amesema

Ametaja wilaya 18 na mikoa nane ya nyanda kame ambazo “ruzuku ndogo isiyozidi Sh.5. milioni itatolewa” kuwa ni; Dodoma (Wilaya za Dodoma na Chamwino); Singida (Wilaya za Ikungi na Singida); Shinyanga (Wilaya za Shinyanga na Kishapu) na Simiyu (Wilaya za Bariadi na Busega).

Zingine ni; Manyara (Wilaya za Babati na Hanang); Arusha (Wilaya za Arumeru, Monduli na Longido), Kilimanjaro (maeneo ya tambarare ya Wilaya za Rombo na Same) na Kagera (Wilaya za Biharamulo, Karagwe na Ngara).

Ally amesema “ili shule ipate ruzuku hiyo inapaswa kutimiza vigezo vyote vya maandiko ya miradi vinavyotumika wakati wa kuchagua miradi itakayopatiwa ruzuku ya mfuko.”

Pia, shule zinapaswa kupata ruksa kutoka kwa wakurungezi wa halmashauri husika, ushauri wa wataalamu wa misitu pamoja na kuwa na maeneo kwa ajili ya uanzishwaji wa vitalu vya miti shuleni na upandaji wa miti.
“Tunaamini shule zitakazofanikiwa kupatiwa ruzuku, zinategemewa kutoa hamasa ya upandaji miti katika shule na vijiji vya jirani.”

Amesema, mwisho wa kupokea maandiko ya miradi inayoomba ruzuku ndogo inayoombwa na shule hizo ni tarehe 30 Juni 2021 kwa awamu ya kwanza na 31 Desemba, 2021 awamu ya pili.”

Ally amesema, mbali ya shule hizo za Nyanda Kame, Mfuko wa Misitu Tanzania unawakaribisha vikundi vya kijamii, asasi zisizo za kiserikali zinazojihusisha na uhifadhi, usimamizi na uendelezaji wa rasilimali misitu kuomba ruzuku hiyo.

“Kipaumbele katika miradi hii watapewa vikundi vya wanawake na vijana wanaojihusisha na ufugaji nyuki inayolenga uhifadhi wa misitu ya asili katika mikoa ya Lindi, Mbeya, Songwe, Rukwa, Tabora, Shinyanga, Kigoma na Katavi,” alisema Afisa huyo wa TaFF,” amesema

Vikundi hivyo, pia vinaweza kupatiwa ruzuku ya fedha kwa ajili ya kugharimia utekelezaji wa shughuli zilizoainishwa kwenye maandiko yao ya miradi pamoja na mafunzo ya kutengeneza mizinga bora ya nyuki.

Katika hatua nyingine, Mfuko wa Misitu unakaribisha maandiko ya miradi kutoka Taasisi za Serikali zikiwemo TFS na Halmashauri za wilaya kuomba ruzuku ya uanzishwaji wa vituo vya ukusanyaji wa asali na mazao mengine ya nyuki.

Ally amesema, mikoa inayopewa kipaumbele katika uanzishwaji wa vituo hivi ni pamoja na mkoa wa Katavi, Rukwa, Geita, Tabora, Kigoma, Singida, Lindi, Mbeya na Songwe.

“Ili kikundi au taasisi iweze kupewa ruzuku inapaswa kutimiza vigezo vyote vya maandiko ya miradi vinavyotumika wakati wa kuchagua miradi itakayopatiwa ruzuku na mfuko,” amesema Ally.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NMB Bonge la Mpango – ‘Moto Uleule’ yazinduliwa, Milioni 180…

Spread the loveMSIMU wa tatu wa Kampeni ya kuhamasisha utamaduni wa Kuweka...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia awataka wahariri kufanya kazi bila uoga, upendeleo

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan amewataka wahariri wa vyombo...

Habari Mchanganyiko

STAMICO yasaini mkataba wa bilioni 55.2 kuchoronga miamba GGML

Spread the loveSHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limezidi kufanya vizuri katika...

Habari Mchanganyiko

NMB yatoa traksuti za Mwenge wa Uhuru Mtwara

Spread the loveBENKI ya NMB imetoa traksuti kwa mkoa wa Mtwara ambako...

error: Content is protected !!