AHADI aliyoitoa Rais wa Tanzania, John Magufuli wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu uliopita mwaka 2020, Itigi mkoani Singida, kwamba atajenga barabara za kilometa 10, imeibuliwa bungeni. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).
Akiuliza kuhusu ahadi hiyo leo Jumatatu tarehe 8 Februari 2021, Yahaya Masare, Mbunge wa Manyoni Magharibi (CCM), ameuliza wakati utekelezaji huo utaanza.
“Wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu 2020, Mhe. Rais akiwa katika Mji wa Itigi, aliahidi ujenzi wa barabara kwa kilometa 10 katika Mji huu. Je,ni lini utekelezaji wa ahadi hiyo utaanza?” ameuliza.
Naibu Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Dk. Festo Dugange amesema, inaendelea kuboresha miundombinu katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo Itigi.

Na kwamba, katika Mwaka wa Fedha 2019/20, serikali ilijenga barabara yenye urefu wa kilometa 1.1 kwa kiwango cha lami kuzunguka Stendi Kuu ya Mabasi, Itigi kwa gharama ya Sh. 499.87 milioni.
“Serikali imekamilisha usanifu wa barabara zenye urefu wa kilomita 10 kwa kiwango cha lami eneo la Itigi, ambazo zitagharimu kiasi cha Sh.9.5 bilioni.”
“Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kutekeleza mradi huo. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2020/21, kiasi cha Sh.686.8 bilioni kimetengwa kwa ajili ya ujenzi na matengenezo ya barabara zenye urefu wa kilometa 101.36 ambapo mpaka sasa kiasi cha Shilingi 253.97 bilioni kimetolewa na utekelezaji unaendelea,” ameema
Leave a comment