February 28, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Sheikh Ponda aibwaga tena Serikali, aachiwa huru

Sheikh Ponda Issa Ponda

Spread the love

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali rufaa ya Serikali dhidi ya Sheikh Issa Ponda, anaandika Faki Sosi.

Katika rufaa hiyo Serikali ilipinga hukumu ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro iliyomuachia huru Sheikh Ponda katika tuhuma ya uchochezi.

Hukumu hiyo imetolewa leo na Jaji Mkasi Mongwa.

error: Content is protected !!