Saturday , 25 March 2023
Home Kitengo Michezo Shabiki wa Yanga awekwa Makumbusho ya Taifa
MichezoTangulizi

Shabiki wa Yanga awekwa Makumbusho ya Taifa

Spread the love

 

SHABIKI wa Yanga, Mansur Hussen aliyetembea kwa miguu kutoka Kigoma hadi Dar es Salaam kwa ajili ya kutazama mchezo wa Simba na Yanga uliokwa ufanyike tarehe 8 Mei, 2021 ameweka vifaa vyake ikiwemo jezi na viatu katika jumba la Makumbusho ya Taifa. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Shabiki huyo alitumia siku 22 kufika Dar es Salaam baada ya kuanza safari ya tarehe 22 Aprili kutoka Kigoma majira ya saa 8 mchana na kufika Dar es Salaam, tarehe 8 Mei, 2021 majira ya saa 1 usiku.

Akipokea vifaa hivyo Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa, amesema Mansur ameweka rekodi ya kufanya hivyo kati ya watu wachache na kumbukumbu wataitambua kama taasisi hiyo.

“Tunatoa pongezi kubwa kwa Mansur kutembea kwa miguu kutoka Kigoma hadi Dar es Salaam, ameweka Historia kati ya watu wachache waliofanya hivyo na historia hii tutaitambua kwenye michezo,” alisema Dk. Noel.

Aidha Dk. Noel aliongezea kwa kuipongeza klabu ya Yanga kwa kuikumbuka Makumbusho ya Taifa kwa kuja kuweka historia hiyo kwa manufaa ya Taifa.

“Niwapongeze Yanga na Mansuri kwa kutambua umuhimu wa kuja Makumbusho ya Taifa, kwa kuja kutoa mchango kwa historia hii iliyowekwa Yanga kwa ajili ya Taifa,” aliongeza mkurugenzi huyo.

Kwa upande wa Mansur, alisema sababu ya msingi iliyomfanya kutembea umbali huo ni kwa ajili ya kuisapoti timu yake ya Yanga kwenye mchezo wao dhidi ya Simba.

“Nimefanya hivyo kwa ajili ya kuisapoti timu yangu ya Yanga na pia kuonesha kuwa mimi ni mwanariadha ninayeweza kwenda masafa marefu,” alisema Mansur.

Licha ya kutembea umbali wote huo mchezo baina ya timu hizo mbili haukufanyika mara baada ya klabu ya Yanga kugomea mabadiliko ya muda yaliyofanywa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kutoka saa 11 jioni hadi saa 8 mchana.

Mara baada ya kuwasili Dar es Salaam, Mansur atarejea nyumbani kwake mkoani Kigoma kwa usafiri wa ndege.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Yanga: Fedha za Rais Samia zinaleta ari kubwa

Spread the loveUONGOZI wa klabu ya Yanga, umesema fedha zinazotolewa na Rais...

Michezo

Simba Sc. yamvulia kofia Rais Samia, yamuahidi makubwa dhidi ya Horoya

Spread the loveWAKATI timu ya Simba ikiibuka na ushindi wa bao 3-0...

Habari MchanganyikoTangulizi

Rais Samia ampandisha cheo RPC wa Dar

Spread the loveMKUU wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Camillus Wambura, amesema...

Habari za SiasaTangulizi

Wanachama 384 CUF watimkia Chadema, Mbowe awapokea, Kambaya ndani…

Spread the loveJUMLA ya wanachama 384 wanachama wa Chama cha Wananchi CUF...

error: Content is protected !!