Sunday , 19 May 2024
Home Gazeti Makala & Uchambuzi Mlinzi wa Rais Obote aliyedhaniwa kufa arejea baada ya miaka 50
Makala & Uchambuzi

Mlinzi wa Rais Obote aliyedhaniwa kufa arejea baada ya miaka 50

Vincet Obodo (katikati) akiwa na wake zake baada ya kurejea
Spread the love

 

MKUU wa zamani wa usalama wa Rais wa Uganda, marehemu Milton Obote, ambaye alidhaniwa amekufa, amerejea nyumbani kwao Uganda baada ya miaka 50 ya kuishi uhamishoni. Anaripoti Saed Kubenea, Dar es Salaam … (endelea).

Vincet Obodo (81), aliyekuwa mkuu wa usalama wa rais wa Obote, alikutana na ndugu zake kwa mara ya mwisho, Januari 1971, wakati serikali ya Rais Obote ilipopinduliwa na Idi Amin Dada.

Familia yake, pamoja na marafiki wengine, walimwaga machozi ya furaha wakati Bw. Obodo aliposindikizwa nyumbani na mfanyakazi wa shirika la wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR), gazeti la Daily Monitor limeripoti.

Obodo alikuwa akiishi uhamishoni nchini Tanzania kwa kipindi cha miongo mitano.

Aliliambia gazeti la serikali la Daily Monitor, kwamba “nimefurahi kurudi nyumbani na kuunga na familia yangu.”

Aliongeza, “maisha ya uhamishoni yamekuwa kichaka cha miiba.”

Rais wa zamani wa Uganda, Marehemu Milton Obote

Rais Obote alipinduliwa na jeshi alipokuwa safarini nchini Singapore, ambako alikwenda kuhudhuria mkutano wa Jumuia ya Madola.

Obodo amesema, wakati huo alikuwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta, nchini Kenya, akisubiri kurudi kwa Rais Obote kutoka Singapore, ndipo alipojua kuhusu kufanyika kwa mapinduzi.

Obote alikwenda uhamishoni Tanzania, na hivyo ndivyo Bw. Obodo alipojikuta Tanzania, na kusalia huko hata baada ya Bw. Obote kurejea tena madarakani mwaka 1980, ingawa alipinduliwa tena mwaka 1985.

Bw. Obodo, ambaye kuna wakati aliwahi kuongoza idara ya ulinzi katika ofisi ya rais, alikutana na wake zake wawili na watoto Ijumaa, iliyopita.

Amin aliiongoza Uganda kwa miaka minane kati ya mwaka wa 1971 hadi 1979, alipopinduliwa na Obote.

Utawala wake, ulishuhudia mauaji ya wapinzani wake wengi. Ametuhumiwa pia kuwatimua wahindi wote nchini Uganda. Aliaga dunia akiwa uhamishoni nchini Saudi Arabia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Makala & UchambuziTangulizi

Askofu Bagonza: Potofu huzaa potoshi/ potoshi huzaa potofu?

Spread the loveDayosisi 7 za KKKT katika kanda ya Ziwa na Magharibi,...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Rais Samia ni Mzanzibari: Shida Iko Wapi?

Spread the loveTAIFA linakabiliwa na upungufu wa fikra sahihi. Upungufu huu unaonekana...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Mpina mwiba CCM, ahofia kuzibwa mdomo

Spread the loveWAKATI Chama cha Mapinduzi (CCM), kikijinasibu kuwa kinara wa demokrasia...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Mabeyo ametuepusha

Spread the loveNIMEGUSWA na uadilifu, utiifu na uaminifu wa Mkuu mstaafu wa...

error: Content is protected !!