Friday , 3 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Mkwamo malori bandari Dar wasimamisha Bunge
Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mkwamo malori bandari Dar wasimamisha Bunge

Malori yakiwa katika foleni ya kuingia bandarini Dar es Salaam
Spread the love

KADHIA ya malori kutoshusha wala kuoandisha mizigo kwa siku tano mfululizo, imelisukuma Bunge kuahirishwa kwa dakika 20 ili kujadili mkwamo huo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Cosato Chumi, Mbunge wa Mafinga Mjini (CCM) ndiyo aliyesimama na kujenga hoja ya kuahirishwa kwa shughuli za bunge ili kujadili mkwamo wa malori Dar es Salaam.

Akijenga hoja leo tarehe 12 Mei 2021, bungeni jijini Dodoma, Chumi amesema, bandari zetu zipo kwenye ushindani lakini akwa siku tano, kuna mkwamo wa kupakia na kushusha mizigo katika bandari ya Dar es Salaam.

“Hatuwezi kukaa kimya tkaacha mambo ya namna hii yaendelee, ndio maana ninajenga hoja, tuahirishe mjadala ili tujadili jambo hili nyeti,” amesema Chumi. Wakati akitoa hoja hiyo, Bunge lilikuwa likiendelea na mjadala wa Wizara ya Afya.

Dk. Tulia Ackson, Naibu Spika

Mbunge huyo, amesema kushindwa kwa malori hayo kushusha na kupakia mizigo, ni sawa na kusimama kwa uchumi “..kwa maana uchumi kwa namna fulani umesimama.”

Ameliambia bunge, katika malori hao kuna inayokwenda katika miradi mbalimbali ya serikali ikiwa ni pamoja na uzalishaji wa umeme wa maji kwenye Bwawa la Mwalimu Nyerere pia ujenzi wa reli ya kisasa (SGR).

Kutokana na hoja hiyo, Dk. Tulia Ackson, Naibu Spika aliruhusu kujadiliwa kwa hoja hiyo kwa dakika 20. Hata hivyo, Jenista Mhagama, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu amesema, Kasim Majaliwa ambaye ni Waziri Mkuu anaelekea Dar es Salaam kutatua mkwamo huo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wadau wataka kasi iongezeke marekebisho sheria za habari

Spread the love  WADAU wa tasnia ya habari wametakiwa kuongeza juhudi katika...

Habari Mchanganyiko

TEF yawatuliza wadau wa habari marekebisho vifungu kandamizi

Spread the love  JUKWAA la Wahariri Tanzania (TEF), limewataka wadau wa habari...

Habari za Siasa

Vijana ACT-Wazalendo Dar wampa tano Rais Samia

Spread the love  NGOME ya Vijana ya Chama cha ACT-Wazalendo, kimempongeza Rais...

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yaiangukia Serikali kunusuru wananchi Liwale, Nachingwea

Spread the love  CHAMA cha ACT-Wazalendo, kimeitaka Serikali kuchukua hatua za haraka...

error: Content is protected !!