Friday , 26 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Serikali yazitia Kitanzi Asasi za kiraia, THRDC watoa kauli
Habari Mchanganyiko

Serikali yazitia Kitanzi Asasi za kiraia, THRDC watoa kauli

Spread the love

MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) umepinga kauli ya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Tixon Nzunda ya kuzuia watendaji wa Serikali kutoa ushirikiano kwa Asasi zisizo za Kiserikali (Azise), anaandika Faki Sosi.

Katibu huyo Novemba 17 mwaka huu akiwa Tabora amenukuliwa akizuiya watendaji wa Serikali za Mitaa kutokubali kutoa ushirikino kwa asasi za kiraia mpaka wapate ruhusa kutoka wizarani (Tamisemi).

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mratibu wa Mtandao huo Onesmo Ole Ngurumwa amesema kuwa kauli hiyo itapelekea kukwamisha kwa shughuli za asasi hizo zenye michango kwenye jamii.

Amesema kuwa madai ya Nzunda kwamba taasisi hizo hufanya matumizi mabaya ya fedha zinatolewa na wafadhili na kwamba madai hayo hayana ukweli.

Ole Ngurumwa ameeleza kuwa Msajili wa Tasisi hizo alifanya uhakiki wa kazi za Taasisi hizo nchi nzima na hakubaini ubadhirifu wa fedha unaodaiwa na Naibu Katibu Mkuu huyo.

Akitoa mfano kazi ya THRDC kwa jamii ni matokeo ya watu kujitambua na kujua haki zao ambayo ndio matarajio ya kazi ya asasi hiyo kuijenga jamii kifikra pevu zitakazozaa matunda ya jamii yenye kujua wajibu na haki zake.

Huku akitanabaisha Asasi nyingine zenye kufanya kazi za ujuzi na kutoa huduma kwa jamii zote zina ulazima wa kushirikiana na Serikali za mitaa bila ya vikwazo.

Amesema kuwa kauli ya Naibu Katibu Mkuu huyo imetolewa kwa matakwa binafsi bila kushirikiana na mamlaka husika na zenye kusajili asasi hizo bila kujua michango ya taasisi hizo katika kuleta maendeleo nchini.

Ameeleza kuwa Watendaji wa Serikali za mitaa wanaweza kuitafsiri vibaya kauli hiyo na kupelekea haki ya taasisi hizo kuzimwa moja kwa moja nchi na kunyimwa haki za kuitumikia jamii ambapo hakutakiuwa ushirikiano kati ya taasisi hizo na Serikali katika masuala ya kimaendeleo.

Amesema kuwa kauli hiyo imepingana na kifungu cha 3(1), (2) ya sheria ya mashirika yasiyo ya kiserikali ya mwaka 2002

Ole Ngurimwa ametoa wito kwa taasisi nyengine kwenye kupinga kauli hiyo pamoja na kuitaka Serikali kutoa ufafanuzi juu ya kauli hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!