November 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mbunge Gama afariki dunia

Spread the love

MBUNGE wa Songea mjini, Leonidas Gama amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Peramiho, anaandika Mwandishi Wetu.

Gama amewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Nachingwea, Newala, Mbeya na Ilala. vile vile amewahi kuwa Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.

Inadaiwa marehemu Gama alianguka nyumbani kwake saa saba usiku juzi huko Likuyu; akapooza upande wa kushoto akawa hajitambui kabisa na akapelekwa hospitali ya Peramiho ambako aliwekewa mashine za kumsaidia kupumua.

error: Content is protected !!