August 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Serikali yatoa ufafanuzi watumishi kukopeshwa magari, wanaotumbuliwa

Waziri wa Fedha na Mpango wa Tanzania, Dk. Mwigulu Nchemba

Spread the love

 

SERIKALI ya Tanzania, imetoa ufafanuzi kuhusu pendekezo lake la kuwakopesha magari watumishi wa umma, pamoja na kusitisha mishahara ya wanaovuliwa nyadhifa zao kwa sababu mbalimbali ikiwemo ukiukwaji wa maadili yao ya kazi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Ufafanuzi huo umetolewa leo Ijumaa, tarehe 24 Juni 2022 na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba, akihitimisha mjadala wa makadirio ya mapato na matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha wa 2022/23, bungeni jijini Dar es Salaam.

Dk. Mwigulu amesema Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan, imependekeza uamuzi wa kuwakopesha magari watumishi wenye sifa, ili kubana matumizi kwa ajili ya kuwapunguzia mzigo wananchi.

“Hatupotezi haki ya mtu, ni kwamba anayepanda daraja anakopeshwa gari yake atalipa mkopo ule kadiri anavyofanya kazi. Lakini atasimamia hivi vingine vinavyotupotezea fedha maana yake dereva akistaafu sababu watakaoajiriwa watakuwa wameshakuwa na magari yao. Maana yake hatuajiri kada hiyo na wala hatufukuzi watu. Tunafanya ili tuwapunguzie Watanzania mzigo na tunakubaliana matumizi hayaendi vizuri,” amesema Dk. Mwigulu.

 

Akitoa ufafanuzi zaidi kuhusu suala hilo, Dk. Mwigulu amesema utaratibu huo utaanza kutumika kwa watumishi watakaopanda daraja baada ya sheria husika kupitishwa.

“Utaratibu huo sio wa siku moja, tunapotengeneza mapendekezo tunatafsiri dira ya Rais Samia anavyowaonea Watanzania huruma ya kubeba mzigo mkubwa. Anataka fedha ziende kwenye maendeleo,” amesema Dk. Mwigului.

Dk. Mwigulu amesema “Serikali ina magari zaidi ya 15,000, hayajanunuliwa yote hata kuondoka kwenye utaratibu huo huondoki siku moja unaenda kwa sheria. Kwamba sheria ikishapita wale watakaofuata baada ya hiyo sheria wataanza kwenda na matakwa ya sheria ya nchi na wala hamna haki ya mtumishi itakayopotea.”

Kuhusu watumishi hasa makatibu wakuu wa wizara, wakurugenzi watendaji wa halmashauri, makatibu tawala wa mikoa na wilaya, ambao teuzi zao zinaenguliwa kurudishwa katika mishahara yao ya zamani, Dk. Mwigulu amesema hatua hiyo inalenga kuimarisha uwajibikaji.

“Maana yake taratibu za uteuzi zifuate umakini lakini yule anayeharibu taratibu za kumuondoa zifuatwe . Sasa kama vitu vyote vimefuatwa wewe umeaminiwa umepata nafasi umekosea taratibu za kutolewa zimefuatwa unataka uendelee kulipwa vilevile kwa fesha za watu wanyonge?” amesema Dk. Mwigulu na kuongeza:

“Waendelee kumlipa aliye kazini na wewe usiwe kazini, lazima tutengeneze utaratibu watu wawe na cha kujutia hivi wanavyoenda sas ahivi hawnaa cha kupoteza yaani mnachukua ka cheo kenu yeye anaendelea kulipwa. Tutatengeneza utaratibu wa kuwajibika wawe na cha kupoteza ili akiaminiwa kwenye majukumu ya umma lazima uwe na cha kupoteza ili ubebe majukumu ya wale unaowahudumia.”

error: Content is protected !!