Sunday , 25 February 2024
Home Habari Mchanganyiko Wanafunzi 2,999 wakosa nafasi kidato cha tano
Habari MchanganyikoTangulizi

Wanafunzi 2,999 wakosa nafasi kidato cha tano

Wanafunzi wa kitado cha nne wakiwa katika chumba cha mtihani. Picha ndogo ni Waziri wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, George Simbachawene
Spread the love

JUMLA ya wanafunzi 2,999 wamekosa fursa ya kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya ufundi kati ya wanafunzi 96,018 waliochaguliwa, anaandika Dany Tibason.

Hayo yalielezwa leo na Waziri wa Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, George Simbachawene akizungumza na waandishi wa habari juu ya matokeo ya kujiunga na kidato cha tano katika mwaka wa 2017.

Simbachawene amesema Jumla ya watahiniwa wa shule 349,524 wakiwemo wasichana 178,775 sawa na asilimia 51.1 na wavulana 170,749 sawa na asilimia 48.9 waliofanya mtihani wa kumaliza kidato cha nne mwaka 2016.

Amesema watahiniwa wakujitegemea waliofanya mtiahani huo mwaka 2016 walikuwa 47,751 wakiwemo wasichana 24,587 sawa na asilimia 51.5 na wavulana 23,164 sawa na asilimia 48.5.

Simbachawene amesema watahiniwa waliofaulu kuanzia daraja la kwanza hadi la tatu ni 96,018  sawa na asilimia 27.60 ya watahiniwa waliofanya mtihani wa Tanzania Bara.

Amesema kutokana na hali hiyo ufaulu katika mwaka 2016 uliongezeka kwa asilimia 3.15 ikilinganishwa na na ufaulu wa mwaka 2015.

Waziri huyo amesema kwa mujibu wa mwongozo wa uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na kidato cha tano mwanafunzi anayeomba kuchaguliwa kuendelea na na kidato cha tano na vyuo vya ufundi ulazimika kujaza fomu ya uchaguzi ambayo ndiyo fomu rasmi ya maombi ya kuchaguliwa.

Amesema kwa kuzingatia utaratibu huo, mfumo wa kielektroniki kwa uchaguzi hutumika kupanga mwanafunzi katika machaguo yake ya masomo na shule kwa kuanzia na chaguo la kwanza hadi la tano kulingana na kiwango cha ufaulu wa mwanafunzi.

Amesema mwongozo huo unaelekeza kwamba, kigezo cha mwanafunzi kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya ufundi ni kwa kuzingatia upatikanaji wa alama AAA  hadi CCD kama Cut Off Point kwenye masomo ya tahasusi.

Msikiliza hapa chini👇👇

Pia amesema kuwa mwanafunzi anatakiwa kupata Crediti 3 na paionti zisizopungua 25 kwenye daraja machaguo yaliyojazwa na mwanafunzi kwenye Selform na nafasi zilizopo katika shule husika.

Simbachawene amesema kuwa wanafunzi waliochaguliwa waliojiunga na kidato cha tano mwaka 2017 wanatoka katika shule za serikali na zisizo kuwa za serikali ambapo shule 351 zikiwemo 17 mpya zimepangiwa wanafunzi.

Kuhusu wanafunzi kuwasili katika shule walizopangiwa Simbachawene alisema kuwa muhura wa kwanza wa kidato cha tano kwa mwaka 2017 utaanza 17 Julai  mwaka huu lakini kwa wanafunzi wanaoingia kidato cha sita watafungua shule Julai 3, mwaka huu.

Aidha amesema kwa wanafunzi ambao wanajiunga na kidato cha tano wanatakiwa kufika katika shule na vyuo vya ufundi walivyopangiwa kabla ya 14 Julai mwaka huu na mwanafunzi yoyote ambaye atashindwa kufika kwa muda huo nafasi yake atapewa mwanafunzi mwingine.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Samia atoa pole ajali iliyoua 25, kujeruhi 21 Arusha

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu...

Habari MchanganyikoTangulizi

25 wafariki dunia katika ajali Arusha

Spread the loveWatu 25 wamefariki dunia papo hapo mkoani Arusha katika ajali...

Habari Mchanganyiko

“Jamii ielimishwe faida za uhifadhi”

Spread the loveWIZARA ya Maliasili na Utalii imesema ili kukabiliana na migongano...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Biteko afuta likizo watumishi Tanesco, bosi Morogoro yamkuta

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dk. Doto...

error: Content is protected !!