Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Serikali yasaini mikataba saba ya ujenzi wa Barabara ya Sh. 3.7 trilioni
Habari za SiasaTangulizi

Serikali yasaini mikataba saba ya ujenzi wa Barabara ya Sh. 3.7 trilioni

Spread the love

SERIKALI ya Tanzania chini ya usimamizi wa Wakala wa barabara nchini (TANROAD) imsaini mitakaba 7 ya ujenzi wa barabara 7 kwa kiwango cha lami zenye urefu wa kilometa 2035 ya  thamani ya shilingi tirioni 3.775 na kukamilika kwa muda wa miaka 4 tangu sasa. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Hayo yameeleza leo tarehe 16 Juni 2023 na Waziri wa Ujenzi na uchukuzi Mhandisi Makame Mbarawa wakati wa uwekaji wa sahihi katika mikataba hiyo iliyofanyika ukumbi wa jakaya Kikwetwe jijini Dodoma.

Mhandisi Mbarawa amesema kuwa katika mwaka wa fedha 2022/23 Wizara ilianza taratibu za manunuzi kwa ajili ya kuwapata Makandarasi wa kujenga kwa kiwango cha lami barabara saba (7) zenye jumla ya kilometa 2,035 kwa kutumia utaratibu wa Engineering, Procurement, Construction and Financing (EPC + F).

Amsema kuwa Barabara hizo zitafungua fursa za kiuchumi katika maeneo zinapopita na kwa Taifa kwa ujumla.

“Hatua iliyofikiwa hadi sasa ni kuwa Makandarasi wa miradi yote saba  (7) wamepatikana ambapo leo hii tumeshuhudia Utiaji Saini wa  mikataba ya kazi za ujenzi wa miradi hiyo.”

Amezitaja barabara hizo kuwa zitajengwa kwa utaratibu huu wa EPC + F ni barabara ya Kidatu – Ifakara – Lupiro – Malinyi – Kilosa  Kwa Mpepo – Londo – Lumecha/Songea (km 435.8), Barabara ya Arusha – Kibaya – Kongwa (km 453.42), Barabara ya Handeni – Kiberashi – Kijungu – Kibaya – Njoro – Olboroti – Mrijo Chini – Dalai – Bicha – Chambolo – Chemba – Kwa Mtoro – Singida (km 384.33).

Amezitaja barabara nyingine kuwa ni barabara ya ya Igawa – Songwe – Tunduma (njia nne) (km 237.9), Barabara ya Masasi – Nachingwea – Liwale (km 175), Barabara ya Karatu – Mbulu – Haydom – Sibiti River – Lalago – Maswa (km 339) na Barabara ya Mafinga – Mtwango – Mgololo (km 81).

Mhandisi Mbarawa amesema kuwa maeneo mengi ambayo barabara hizi zitapita yana rasilimali nyingi ambazo hazichangii ipasavyo katika uchumi wa nchi kama inavyopaswa kuwa kwa kutofikika kirahisi kutokana na ukosefu wa barabara zinazopitika wakati wote wa mwaka.

“Hivyo, Serikali inafanya jitihada za makusudi kuhakikisha kuwa maeneo yote ya kimkakati kiuchumi yanafikika kwa urahisi ili kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi wa nchi yetu.

“Aidha, barabara hizi zitachochea kiu ya matumizi ya bandari zetu kwa nchi jirani za Zambia, Malawi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Zimbabwe, Uganda, Rwanda, Burundi na Sudan ya Kusini hivyo kuinua ukuaji wa makusanyo ya fedha kupitia Bandari zetu” ameeleza Mhandisi Mbrawa.

Aidha Mhandisi Mbarawa ameeleza kuwa barabara hizo zitarahisisha usafiri wa wananchi na usafirishaji wa mazao ya misitu, mazao ya biashara, mazao ya chakula, mazao ya uvuvi na ufugaji, malighafi za madini kama vile makaa ya mawe, grafaiti na chuma kutoka mikoa ya Kusini kwenda katika masoko ya ndani na nje ya nchi na kuchochea kasi ya uzalishaji wa mazao hayo na ongezeko la mapato ya Serikali.

Akizungumzia faida za barabara hizo amesema kuwa barabara hizo zitachochea kiu ya matumizi ya bandari za Tanzania kwa nchi jirani za Zambia, Malawi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Zimbabwe, Uganda, Rwanda, Burundi na Sudan ya Kusini hivyo kuinua ukuaji wa makusanyo ya fedha kupitia Bandari zetu.

Ameeleza kuwa Serikli inatarajia ujenzi wa barabara hizo utakapokamilika, maeneo yote yenye mikakati mizuri ya kiuchumi yatavutia kwa kiwango kikubwa uwekezaji wa ndani na kimataifa na kuzalisha ajira kwa Watanzania. 

Amesema kuwa ujenzi wa barabara hizo utatoa ajira za moja kwa moja kwa Watanzania takribani 20,300, huku Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi imebuni mkakati wa kupunguza tatizo la ajira na kuwajengea uwezo wa kitaalam wahitimu wa vyuo vikuu kwa kuweka masharti ya kuajiri wahitimu hao katika Mikataba ya Ujenzi na Usimamizi ambapo wahitimu wasiopungua 70 watapata ajira.

Utaratibu huu tutauendeleza katika miradi mingine mipya inayotekelezwa kupitia Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, na kuziomba Taasisi zingine za umma zifikirie kupunguza wimbi la wahitimu wasio na ajira kwa utaratibu huu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

Habari za Siasa

Serikali yasaka bilioni 3 kujenga daraja Mto Mpiji

Spread the loveSerikali imesema inaendelea na juhudi za kutafuta fedha kiasi cha...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kwafukuta kisa chaguzi, Lissu aibua tuhuma nzito

Spread the loveCHAGUZI za kusaka viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo...

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga “HIDAYA” chaendelea kuimarika, wananchi wapewa tahadhari

Spread the loveMAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kutoa taarifa...

error: Content is protected !!