Sunday , 19 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Serikali yapongeza Dira ya miaka 50 CBE
Habari Mchanganyiko

Serikali yapongeza Dira ya miaka 50 CBE

Spread the love

SERIKALI imekitaka Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), kuweka mikakati ya kujiimarisha kiteknolojia, uvumbuzi na ubunifu ili kuendana na mahitaji ya soko la ajira ambayo yanakwenda kwa kasi.

Wito huo ulitolewa leo jijini Dar es Salaam  na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dk. Hashil Abdallah, wakati wa mjadala wa Dira ya Maendeleo ya miaka 50  ya chuo hicho itakayotekelezwa hadi mwaka 2074. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Alisema chuo hicho kinapaswa kutoa elimu ambayo itakidhi mahitaji ya soko la ndani na nje ya nchi kwa kuwa na wahitimu wenye weledi wa kutosha kupokelewa na waajiri popote watakapokwenda.

Alisema sekta ya biashara ni kiungo muhimu katika kukuza biashara nchini na kukuza uchumi hivyo sekta hiyo inapaswa kutoa elimu bora kwani ndio msingi wa maendeleo ya  uchumi nay a kijamii.

Alikipongeza chuo hicho kwa kuendelea kufanya mageuzi yanayoendana wakati na teknolojia katika fani ya biashara na juhudi zake za kujenga uwezo wa kitaaluma na kiufundi kwa wanafunzi wa chuo hicho.

“Dira ya miaka 50 ya chuo cha CBE ambayo imeandaliwa kwa umahiri mkubwa na kwa kushirikisha wadau mbalimbali ni hatua muhimu katika kuhakikisha chuo hiki kinabaki kuwa imara katika kutoaelimu bora na kusaidia ukuaji wa biashara,” alisema

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dk. Hashil Abdallah akizungumza na Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Bishara CBE leo kwenye uzinduzi wa Dira ya Maendeleo ya miaka 50 ya Chuo cha Elimu ya Biashara CBE katika ukumbi wa JNICC Dar es Salaam

Alisema ni matumaini ya serikali kuwa iwapo dira hiyo itatekelezwa kwa ufasaha itasaidia kuleta mabadiliko makubwa kwenye sekta ya biashara na kwenye jamii kwa ujumla.

Alisema chuo hicho kinapaswa kuwa tayari kukabiliana na changamoto zinazoweza kujitokeza katika taasisiz a elimu ili kiwe na uwezo wa kubailika kwa haraka kukidhi mahitaji ya soko la ajira.

Mkuu wa chuo hicho, Profesa Edda Lwoga, alisema katika kampasi zake zote chuo hicho katika mikoa ya Dar es Salaam, Mbeya, Mwanza na Dodoma  kina jumla ya wanafunzi 19,000 na kwamba wamekuwa wakijitahidikutoan elimu kwa vitendo zaidi.

Aidha, alisema katika kutekelez dira yake ya miaka 50 walishaanza kufanya mageuzi ya kutoa nelimu kwa vitendo ambapo walifanikiwa kuanzisha program za uanagenzi ambapo wanafunzi husoma wakiwa wanafanyakazi kwa vitendo.

“Na napendaa kutoa taarifa kuwa tumeshapata ithibati ya program za uanagenzi na mwaka huu tutaanza na kozi za benki na metrolojia ambapo watakuwa nusu shuleni na nusu watakuwa kazini,” alisema Profesa Lwoga.

Katibu Mkuu akiteta jambo na Mkuu wa chuo, Profesa Edda Lwoga leo baada ya uzinduzi wa mjadala wa miaka 50

Alisema kwenye kozi ya metrolojia watashirikisha n Wakala wa Vipimo (WMA), ambapo wanafunzi watakuwa darasani kwa muda na watakwenda kufanyakazi.

Alisema CBE ilishaanzisha program atamizi kwa wanafunzi wenye ndoto za kuanzisha biashara kupelekwa mawazo yao ambayo huboreshwa na kupewa mafunzo ambayo hatimaye huwawezesha kufanya biashara hizo.

“Tumeshaanza sasa ni miaka miwili na wanafunzi wengi wameshajitokeza kusajili biashara na kampuni zao wakiwa bado chuoni na katika kuendana na mabadiliko ya teknolojia tumeshaanzisha masomo ya mtandao,” alisema

Profesa Lwoga alisema kwa kuanza wameanza kutoa Shahada sita za Uzamili kwa njia ya mtandao na kwamba wataongeza kozi ya biashara ya kimataifa na kozi ya ununuzi na ugavi.

“Tumeona mwitikio ni mkubwa sana kwasababu wanafunzi wetu popote pale walipo watajisajili kwa njia ya mtandao na watalazimika tu kuja hapa chuoni kwa ajili ya mitihani ya majaribio tu na mitihani ya mwisho,” alisema

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dk. Hashil Abdallah akizungumza leo kwenye uzinduzi wa Dira ya Maendeleo ya miaka 50 ya Chuo cha Elimu ya Biashara CBE katika ukumbi wa JNICC Dar es Salaam

Alisema dira yao ya miaka 50 inawakilisha maono ya wanafunzi na wadau wote wa chuo hicho kwani chuo kimejitahidi kushirikisha maoni ya watu wengi wakati wa kuandaa dira hiyo.

Alisema miongoni mwa sababu zilizochochea chuo hicho kuandaa dira hiyo ni mabadiliko ya teknolojia kama akili bandia, roboti na utandawazi.

“Tulifikiri namna gani ya kufanya chuo chetu kwenda kimataifa zaidi na kuendana na matarajio ya wanafunzi wetu, mabadiliko katika jamii na mabadiliko ya kiuchumi kwa hiyo tunapaswa kujenga miundombinu imara ya kiteknolojia kuendeleza program za mafunzo zinazotekeleza teknolojia ya kisasa,” alisema

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

CCM yamteua Pele kuwa mgombea ubunge Kwahani

Spread the loveKamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Canada yatenga bilioni 38 kutekeleza mradi ya kuinua vijana TZ

Spread the loveSERIKALI ya Canada kupitia ‘CARE International Canada’ imetenga takribani Sh...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Ujenzi kituo cha kupoza umeme Chalinze wafikia asilimia 93.7

Spread the loveKamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeeleza...

Habari Mchanganyiko

Balile ateuliwa rais wa wahariri Afrika Mashariki

Spread the loveJumuiya ya Wahariri wa Afrika Mashariki (EAES), imemchagua Mwenyekiti wa...

error: Content is protected !!