Sunday , 19 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Wafugaji Igunga wachagua viongozi, matapeli waonywa
Habari Mchanganyiko

Wafugaji Igunga wachagua viongozi, matapeli waonywa

Spread the love

Chama cha wafugaji wilaya ya Igunga mkoani Tabora kimefanya uchaguzi wa viongozi ngazi ya kata  na wilaya watakaoongoza kwa kipindi cha miaka mitatu. Anaripoti Abdallah Amiri, Tabora … (endelea).

Uchaguzi huo ulifanyika katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Igunga ambapo ulihudhuriwa na wajumbe 217 wa kata 35 za wilaya ya Igunga waliochaguliwa ngazi ya kata ambao ni wafugaji.

Viongozi waliochaguliwa ngazi ya wilaya ni pamoja na mwenyekiti wa wafugaji Mafunda Jing’weka Temanya ambaye pia ni mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Igunga na Makamu mwenyekiti Gandu Daud Kulwa.

Viongozi wengine ni Katibu wa wafugaji (wilaya ya Igunga) Johari Jumanne Kaduguda, Katibu msaidizi Getrude Gitang Matofali.

Baadhi ya viongozi wa wafugaji waliochaguliwa ngazi ya wilaya ya Igunga mkoani Tabora wa kwanza kulia Johari Jumanne Kaduguda ambaye ni Katibu wa wafugaji (wilaya ya Igunga) wa katikati Mwenyekiti wa wafugaji wilaya ya Igunga Mafunda Jing’weka Temanya ambaye pia ni mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Igunga na wa tatu kushoto Makamu mwenyekiti Gandu Daud Kulwa wote wakiwa wamesimama.

Mweka hazina wa wafugaji wilaya ya Igunga, Jagila Makinda Baya na Mjumbe wa mkutano wa wafugaji Taifa Ginang Kitabeka Gambeshi.

Wajumbe wa kamati tendaji ya wafugaji wilaya ya Igunga ni Lucas Mashauri Butoga (ambaye pia ni Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Igunga), Jolomogo Mashala Mawe, Kasala Lubinza Luhanga, Musa Elias Kazwenge na John Enock Nkuba.

Akitoa shukrani za kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa wafugaji wa wilaya ya Igunga, Mafunda aliwahakikishia wafugaji kuwa changamoto zote ambazo zitakuwa zikijitokeza zinazowahusu wafugaji atazishughulikia akishirikiana na serikali.

“Ndugu zangu wafugaji leo tumemaliza uchaguzi naomba niwambie bila kuogopa kuna baadhi ya matapeli wamekuwa wakipita kwa wafugaji na kuwachukulia fedha wakiwaaminisha kuwa watawatatulia kero zao wakati wao hawana uwezo.

“Hivyo basi napenda kuwaambia wale wote wenye tabia hiyo waache mara moja na wasipoacha basi wahame Igunga mimi siko tayari kuona wafugaji wakitapeliwa nitatumia vyombo vya usalama kuwasaka popote walipo,” alisema Mafunda huku akishangiliwa na wafugaji.

Aidha, Mafunda waliwaomba wafugaji wote kuendelea kujisajili kwa njia za kielektroniki ili waweze kutambulika kisheria ambapo itarahisisha Serikali kuwapelekea huduma zao za kijamii.

Wakati huo huo Mwenyekiti huyo aliwaomba viongozi wote waliochaguliwa ngazi ya kata na wilaya kusoma mapato na matumizi ikiwa pamoja na kukutana na wafugaji kusikiliza kero zao.

Sanjari na hayo, mwenyekiti huyo aliwaomba viongozi wa wafugaji taifa kufikisha salamu kwa Rais Samia Suluhu Hassani kuwa wafugaji Igunga wataendelea kushirikiana na serikali kwa shughuli zote na maelekezo yote yatakayotolewa na Rais.

Viongozi waliohudhuria ngazi ya Taifa ni pamoja na Joji Simon Kifuko Mjumbe wa tume ya uchaguzi, Godfrey Maige Katuba mjumbe wa sekretaleti ya uchaguzi na Thomas Manyanda Kapomole mkuu wa itifaki taifa.

Akizungumza kwa niaba ya viongozi wenzake mjumbe huyo wa tume ya uchaguzi wa Chama cha wafugaji Taifa Joji Kifuko aliwaambia wafugaji hao kuwa lengo kubwa la kufanya uchaguzi ni kupata viongozi wa kila kata, wilaya, mkoa hadi taifa.

Wafugaji kutoka kata 35 za wilaya ya Igunga mkoani Tabora waliochaguliwa kuongoza ngazi ya kata wakiwa katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Igunga wakishiriki uchaguzi wa kuchagua viongozi 11 ngazi ya wilaya.

Alisema mwaka 2013 – 2014 kulikuwa na kauli isemayo “tokomeza majangili” lakini baadae ikawa tokomeza wafugaji hali ambayo ilifanya wafugaji waliopo jirani na hifadhi kuishi kwa misuko suko ikiwa ni pamoja na kupoteza mifugo yao.

Kifuko alisema kufuatia hali hiyo wao walipeleka malalamiko yao bungeni kwa kuwa serikali ni sikivu mawaziri wanne waliondolewa madarakani hata hivyo hakuwataja majina yao.

Alisema endapo tutakuwa na uongozi wa wafugaji kwa nchi nzima itasaidia kushirikiana na serikali kutatua migogoro ya wafugaji ambayo imekuwa ikitokea baadhi ya maeneo hapa nchini.

Aidha, mjumbe huyo wa tume ya uchaguzi alitumia nafasi hiyo kwa kuwaasa wafugaji wote nchini kujiepusha kutengeneza migogoro isiyokuwa ya lazima na badala yake wazingatie sheria za nchi pindi wanapokumbana na changamoto za mifugo yao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

CCM yamteua Pele kuwa mgombea ubunge Kwahani

Spread the loveKamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Canada yatenga bilioni 38 kutekeleza mradi ya kuinua vijana TZ

Spread the loveSERIKALI ya Canada kupitia ‘CARE International Canada’ imetenga takribani Sh...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Ujenzi kituo cha kupoza umeme Chalinze wafikia asilimia 93.7

Spread the loveKamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeeleza...

Habari Mchanganyiko

Balile ateuliwa rais wa wahariri Afrika Mashariki

Spread the loveJumuiya ya Wahariri wa Afrika Mashariki (EAES), imemchagua Mwenyekiti wa...

error: Content is protected !!