Sunday , 3 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Serikali yaja na vifaa vya kisasa vya upimaji ardhi
Habari za Siasa

Serikali yaja na vifaa vya kisasa vya upimaji ardhi

Spread the love

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amesema, wizara yake imeleta Vifaa vya kisasa vya upimaji wa ardhi ambavyo vitagawiwa kwa ofisi zote za kanda za ardhi nchini ili halmashauri zote nchini ziweze kutumia. Anaandika Faki Sosi … (endelea).

Vifaa hivyo ambavyo vipo kwa Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani wa Wizara ya Ardhi, vitatumika nchi nzima ili kila Taasisi, Mkoa, Wilaya, Makampuni Binafsi na yeyote yatakaye vihitaji vitatumika bila gharama.

Aidha Waziri Lukuvi amesema vifaa hivi vitatumiaka pia katika utatuzi wa migogoro ya ardhi pale vitakapohitajika, hasa katika migogoro ya Wananchi na Hifadhi za Taifa.

Amesema Wizara yake ameagiza vifaa hivyo kwa wingi ili kuhakikisha nchi nzima inapimwa na kupangwa na kuepusha migogoro ya ardhi ambalo ndio jukumu lake kubwa alilopewa na Mheshimiwa Rais katika miaka mitano hii.

Waziri Lukuvi ameyasema hayo wilayani Babati mkoani Manyara alipokuwa akizindua rasmi mpango wa utekelezaji wa matumizi bora ya ardhi ya vijiji vinavyopakana na hifadhi za taifa.

Mpango huu unatekelezwa na Hifadhi za Taifa Tanzania ambayo ipo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa ushirikiano na Tume ya Taifa ya Mpango wa Matumizi ya Ardhi ambayo ipo chini ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Mpango huu umekusudia kupima vijiji vyote 392 vinavyozungika hifadhi nchi nzima hasa katika mikoa ya Arusha, Manyara na Mara.

Mpango huu ni Ushirikiano kati ya Wizara hizi mbili ili kuondoa kabisa migogoro ya ardhi iliyopo kati ya wananchi na hifadhi zinazo wazunguka.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Dk. Biteko aagiza wakurugenzi TANESCO kukemea rushwa kwenye maeneo yao

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Uongozi wa Samia kuendelea hadi 2030

Spread the loveKWETU sisi tuliowahi kusoma sekondari, iwe O levo au A...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Bado askari wastaafu wanaonewa

Spread the loveRAIS wangu Samia Suluhu Hassan tunaendelea kumshukuru Mungu kwamba wote...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Tunastawisha ufisadi na kuchukia matunda yake

Spread the loveBUNGE la Jamhuri linaloendelea mjini Dodoma, kwa wiki nzima limetawaliwa...

error: Content is protected !!