February 26, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Moto wateketeza mali za mamilioni Ngara

Spread the love

MAGARI matano ya mizigo, yameteketea kwa moto katika kituo cha forodha kilichomo eneo la Rusomo, wilayani Ngara, mpakani mwa Tanzania na Rwanda, leo Jumapili, tarehe 19 Agosti 2018. Anaripoti Mwandishi Wetu kutoka Rusomo … (endelea).

Taarifa kutoka kwa mashuhuda wa tukio hilo zinasema, magari hayo yameteketea kwa moto kufuatia gari moja lililobeba mafuta aina ya petroli kuligonga gari jingine, lililokuwa limeegeshwa katika eneo hilo.

“Ni kweli tukio hilo limetokea kwenye eneo hili. Gari tano ambazo zilikuwa zimeegeshwa kusubiri ruhusa ya kuvuka mpaka, zimeteketea kwa moto,” anasimulia Nyungura Ndyekimana, mfanyabiashara wa Rusomo na raia wa Rwanda.

Anasema, “athari za ajali hii zimekuwa kubwa zaidi kutokana na kukosekana kwa miundo mbinu ya kukaribia na ajali za moto, kama vile gari la zimamoto, ukosefu wa barabara za dharura na kukosekana umakini kwa watu wanaoshughulika na forodha.”

error: Content is protected !!