Friday , 26 April 2024
Home Kitengo Maisha Elimu Serikali ya Tanzania: Hatuajiri walimu wa sanaa
ElimuTangulizi

Serikali ya Tanzania: Hatuajiri walimu wa sanaa

Spread the love

SERIKALI ya Tanzania imesema, itawaajiri walimu wa masomo ya sanaa  pale idadi ya walimu wa sayansi, hisabati, kilimo, biashara, elimu maalum na mafundi sanifu wa maabara za shule za Sekondari itakaporidhisha. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Serikali imetoa majibu hay oleo Jumatatu tarehe 8 Juni 2020 wakati ikijibu swali la Mbunge wa Korogwe Mjini (CCM), Mary Chatanda aliyeuliza kwa njia ya mtandao wa Bunge la Tanzania na kujibiwa kwa mfumo huohuo.

Chatanda ameuliza, “wahitimu wa kada ya walimu wa masomo ya Arts (sanaa) ngazi ya stashahada na shahada kuanzia mwaka 2015 hadi leo hawajapata ajira. Je, nini hatima ya walimu wa kada hizi.”

Akijibu swali hilo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bira amesema, katika utumishi wa umma, nafasi za ajira za watumishi wa kada mbalimbali wakiwemo walimu hutengwa kulingana na vipaumbele vya Serikali.

Amesema, katika miaka ya nyuma ambapo watumishi wa umma wenye sifa walikuwa wachache, Serikali ilitoa ajira za moja kwa moja kutoka vyuoni (direct entry) kwa kada zote.

Waziri huyo amesema, kutokana na watumishi wa kutosha na ili kupata watumishi wenye sifa, weledi na uadilifu, Serikali ilibadilisha utaratibu wa ajira za moja kwa moja na kuanza kutoa ajira kwa njia ya ushindani kupitia usaili wa watumishi wa kada mbalimbali isipokuwa walimu na watumishi wa kada za afya.

“Katika miaka ya hivi karibuni, utumishi wa umma umekabiliwa na changamoto kadhaa ikiwa ni pamoja na kukosekana kwa baadhi ya kada katika soko la ajira hususani kwa baadhi ya kada za afya na elimu (masomo ya sayansi).”

“Kutokana na changamoto hii, Serikali imeweka kipaumbele cha ajira mpya kwa walimu wa masomo ya sayansi, hisabati, kilimo, biashara na elimu maalum pamoja na fani ya fundi sanifu wa maabara za shule,” amesema

Katika majibu hayo, Waziri amesema, kutokana na kuwepo kwa walimu ziada wa masomo ya sanaa katika shule za sekondari hususan maeneo ya mijini, Serikali iliwaagiza waajiri kwenye mamlaka za serikali za mitaa kufanya tathmini ya mahitaji halisi ya walimu na kuhamishia walimu wa ziada katika Shule za Msingi na maeneo yenye upungufu mkubwa wa walimu ili kuweka uwiano mzuri wa walimu kwa wanafunzi.

“Ninapenda kuliarifu Bunge lako Tukufu kuwa, Serikali itaajiri walimu wa masomo ya sanaa pale idadi ya walimu wa masomo ya sayansi, hisabati, kilimo, biashara, elimu maalum na mafundi sanifu wa maabara za shule katika shule za sekondari itakaporidhisha,” amesema

“Aidha, wakati Serikali ikiendelea na mchakato wa kujaza nafasi za walimu wa sayansi, wahitimu wa kada ya ualimu wa masomo ya sanaa wanahimizwa kutafuta ajira katika taasisi nyingine za umma na shule binafsi,” ameongeza

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za SiasaTangulizi

Shibuda amlima waraka mzito Bulembo

Spread the loveMKONGWE wa siasa nchini, John Shibuda amemshukia kada maarufu wa...

error: Content is protected !!