April 13, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Serikali kutoa ruzuku kwa halmashauri

Mwita Waitara, Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais-TAMISEMI

Spread the love

SERIKALI imesema, inaendelea kutoa ruzuku ya maendeleo kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa ili kuziwezesha kutekeleza miradi ya maendeleo katika sekta mbalimbali zikiwemo afya na elimu. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 14 Mei 2019 bungeni na Naibu Waziri Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mwita Waitara alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Leah Komanya (CCM).

Katika swali lake, Komanya alidai kwamba, moja ya kati ya vigezo vya ‘Capital Development Grant Assessment’ ni namna gani halmashauri inaweza kutoa taarifa kwa wananchi, juu ya mtiririko wa fedha ambazo serikali imepeleka katika halmashauri na miradi inayokusudiwa kutekelezwa.

“Je, kwanini mchakato huo ulisitishwa? Je, serikali haioni umuhimu wa kurejesha mchakato huo ambao utakuwa ukiongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya halmashauri nchini?” aliuliza Komanya.

Akijibu Waitara amesema, upimaji wa halmashauri ulikuwa ni kigezo cha kuziwezesha halmashauri kupata ruzuku ya maendeleo isiyo na masharti ‘Local Government Develeopment Grant’ kuanzia mwaka 2005.

“Miongoni mwa vigezo vilivyozingatiwa ni kuwepo kwa uwazi katika mapokezi na matumizi ya fedha kwenye ngazi za vijiji, kata na mitaa kwa kuhakikisha mapato na matumizi yanayobandikwa kwenye mbao za matangazo,” amesema.

Alisema serikali, inaendelea kutoa ruzuku ya maendeleo kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa ili kuziwezesha kutekeleza miradi ya maendeleo katika sekta mbalimbali  zikiwemo afya na elimu.

“Wananchi wanachangia nguvu kazi na vifaa mbalimbali kwa ajili ya ukamilishaji wa miradi hiyo

error: Content is protected !!