March 1, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Serikali kufuatiliwa sakata la watumishi wa CPJ

Dk. Hassan Abbas, Msemaji wa Serikali

Spread the love

MKURUGENZI wa Idara ya Habari Maelezo, Dk. Hassan Abbas amesema ofisi yake inafuatilia sababu ya watumishi wawili wa Kamati ya Kimataifa ya Kuwalinda Waandishi wa Habari (CPJ), kushikiliwa na kuhojiwa na watu wanaodaiwa kuwa maofisa wa Idara ya Uhamiaji nchini. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Dk. Abbas ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali katika ukurasa wake wa Twitter ameandika kuwa “Ofisi yangu inafuatilia kujua kwa nini wanaoitwa waandishi wa habari wa CPJ waliruhusiwa kuingia nchini lakini baadaye wakalazimika kuhojiwa na uhamiaji na kuachiwa.”

Watumishi hao ni Mratibu wa Programu Barani Afrika, Angela Quintal na Mwakilishi wa CPJ Kusini mwa Jangwa la Sahara, Muthoki Mumo wameachwa huru baada ya kushikiliwa na Idara ya Uhamiaji, vile vile, taarifa zinaeleza kuwa, hati zao za kusafiria pia wamerudishiwa.

Watumishi hao walikamatwa usiku wa Jumatano wakiwa kwenye hoteli ya Southern Sun na watu wanaodaiwa kuwa maofisa wa serikali, na kuachwa huru baada ya kuhojiwa kwa saa kadhaa.

error: Content is protected !!