Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbowe, Matiko kukamatwa
Habari za SiasaTangulizi

Mbowe, Matiko kukamatwa

Pingu
Spread the love

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeamuru kumatwa kwa Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa  Chama  cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Ester Matiko, Mbunge wa Tarime Mjini. Anaripoti Faki Sosi… (endelea).

Hakimu Mkazi Mkuu Wilbard Mashauri  leo tarehe 8 Novemba mwaka 2018  ameamuru kukamatwa kwa viongozi hao kutokana na kushindwa kuhudhuria kwenye kesi inayowakabili hapo bila ruhusa ya mahakama.

Taarifa kutoka ndani ya Chadema zinaeleza kuwa, Mbowe amwekenda nchini Afrika Kusini kwa matibabu. Pia mahakamani hapo mdhamini wa kiongozi huyu ameeleza kuwa, yupo nje ya nchi kwa matibabu.

Mdhamini wa Matiko ameieleza mahakama kuwa, mshtakiwa amepata ziara ya kibunge na yuko nchini Burundi pamoja na kuwasilisha vielelezo ikiwamo tiketi ya ndege.

Kesi inayowakabili Mbowe na viongozi wengine waandamizi ni kufanya maandamano yasiyokuwa ni kufanya maandamano bila kibali.

Viongozi wengine kwenye kesi hiyo ni pamoja na Dk. Vicent Mashinji Katibu Mkuu wa Chama Hicho ,Peter Msigwa Mbunge Iringa Mjini, Halima Mdee, Mbunge wa Kawe John Mnyika (Mbunge Kibamba)).

Wengine ni Salum Mwalimu Naibu Katibu wa Chama hicho Zanzibar , John Heche Mbunge wa Tarime Vijijini. na Easter Bulaya (Mbunge Bunda.

Wakati huo huo Wakili Jamhuri Johnson, anayemtetea Mchungaji Peter Msigwa, katika kesi ya uchochezi inayowakabili viongozi tisa wa Chadema, ametangaza kujiondoa kumtetea kwa madai ya kutorishishwa na mwenendo wa kesi hiyo unavyoendeshwa.

Wakili Johnson amedai kuwa, mwenendo wa kesi hiyo hauridhishi na kwamba hajawahi kukutana na kesi ya namna hiyo kwa miaka 20 ya uwakili wake.

Watuhumiwa wote wamegoma kujibu chochote wakati walipokuwa wakisomewa maelezo ya awali kwa madai hawawezi kueleza chochote kutokana na kutokuwa na wakili wa kuwatetea.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!