Wednesday , 29 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Prof. Kabudi aukimbia mtego wa Zitto
Habari za SiasaTangulizi

Prof. Kabudi aukimbia mtego wa Zitto

Spread the love

WAZIRI wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi ameshindwa kujibu kipengele B kwenye swali la Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe kuhusiana na idadi ya mashauri yaliyofunguliwa katika mahakama za kimataifa, ambayo serikali imeshinda na kushindwa. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Zitto leo tarehe 9 Novemba 2018 amehoji bungeni kuwa, “Je kuanzia mwaka 2000 hadi 2018 kumekuwa na mashauri mangapi dhidi ya Jamhuri ya Muungano, mangapi yameamuriwa, mangapi bado na mangapi Tanzania ilishinda.”

Lakini Prof. Kabudi hakujibu swali hilo, akisema kwamba ni la mtego na hivyo hatauingia kamwe mtego huo.

Prof. Kabudi ameeleza kuwa, serikali haita tamka chochote kuhusu kesi zilizofunguliwa kwenye mahakama za kimataifa, kwa kuwa ikitoa tamko na kuingia katika taarifa za bunge (Hansard) litahatarisha hoja za serikali katika kesi hizo.

“Masuala yote aliyoyasema, yale yaliyo katika mahakama za kimataifa serikali haitamka chochote. Nataka niwambie katika sheria za kimataifa tamko lolote nitakalolifanya hapa likaingia kwenye hansard litahatarisha hoja za serikali kwenye kesi hizo, na mtego huo uwe wa bahati mbaya au wa kutumwa sitaungia kamwe,” amesema Prof. Kabudi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

DC Kasilda Mgeni ahamasisha chakula shuleni

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni...

Habari za Siasa

Bilioni 223.9 zapelekwa Tunduru ndani ya miaka 2 ya SSH

Spread the love  ZAIDI ya Sh. bilioni 223.9 zimepelekwa Wilaya ya Tunduru...

Habari za Siasa

Rais Samia aagiza iundwe kamati ya pamoja ya Mawaziri mradi wa BBT

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewaagiza mawaziri kuunda kamati...

Habari za Siasa

Rais Samia apangua makatibu tawala mikoa, ateua Kamishna DCEA

Spread the loveALIYEKUWA Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, Gerald...

error: Content is protected !!