December 1, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Serengeti kinara tena Afrika

Serengeti

Spread the love

 

HIFADHI ya Taifa ya Serengeti iliyopo nchini Tanzania imeshinda tuzo ya kuwa hifadhi bora katika Bara la Afrika kwa mwaka 2021. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Hii ni mara ya tatu mfululizo kwa hifadhi hiyo ya Serengeti kushinda tuzo hiyo.

Tarifa iliyotolewa leo tarehe 21 Oktoba, 2021 na Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Pascal Shelutete imesema tuzo hiyo imetolewa na taasisi ya World Travel Awards (WTA) ya nchini Marekani ambayo ndiyo muandaaji wa tuzo hiyo kila mwaka.

Taarifa hiyo imesema kwa mara ya kwanza Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ilishinda tuzo hiyo ya kuwa hifadhi bora katika bara la Afrika mwaka 2019 na kwa mara ya pili ilikuwa mwaka 2020.

Hifadhi hiyo inayopatikana katika mikoa ya Arusha, Mwanza, Mara pamoja na Shinyanga, katika kipengelea hicho imezishinda hifadhi za Central Kalahari Game Reserve ya Botswana na Etosha Nationa Park ya Namibia.

Nyingine ni Kidepo Valley Nationa Park ya Uganda, Kruger National Park ya Afrika Kusini na Maasai Mara Nationa Rserve ya Kenya.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, zaidi ya aina 70 za wanyama na aina 500 za ndege wanapatikana katika hifadhi hiyo iliyo na sifa ya kipekee duniani ikiwamo misitu na majani ya malisho ya wanyama.

error: Content is protected !!