Wednesday , 24 April 2024
Home Habari Mchanganyiko RC Rukwa anusa ubadhirifu milioni 60 ujenzi kituo cha afya
Habari Mchanganyiko

RC Rukwa anusa ubadhirifu milioni 60 ujenzi kituo cha afya

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Joseph Mkirikiti
Spread the love

 

MKUU wa Mkoa wa Rukwa, Joseph Mkirikiti ameeleza kutoridhishwa na matumizi ya zaidi ya Sh milioni 60 katika ujenzi wa Kituo kipya cha Afya cha Kasu wilayani Nkasi. Anaripoti Raheem Secha, Rukwa … (endelea).

Mkirikiti ametoa kauli hiyo leo tarehe 21 Oktoba, 2021 katika ziara ya aliyoanza mkoani humo kukagua miradi ya maendeleo.

Kutokana na hali hiyo amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri  hiyo, William Mwakalambile kusimamia ipasavyo matumizi ya fedha za serikali zilizoelekezwa mkoani humo kutekeleza miradi mbalimbali ikiwamo kituo hicho cha afya.

Akiwa kwenye eneo la mradi, Mkuu huyo wa mkoa alibaini matumizi yasiyo sahihi ya Sh milioni 60 zilizotumika kati ya Sh milioni 500 zilizotolewa na Serikali kujenga jengo la wagonjwa wa nje.

“Sijafurahishwa na mwenendo wa kazi ya ujenzi hapa. Inaonekana halmashauri hamjajipanga kukamilisha mradi huu unaosubiriwa mno na wananchi” amesema Mkirikiti

Amesema Serikali ilitoa Sh milioni 500 kwa halmashauri ya wilaya ya Nkasi kwa ajili ya ujenzi wa kituo kipya cha Afya Kata ya Kasu ambapo tayari kimeanza kujengwa kwa halamshauri kukusanya vifaa vya kazi.

Kwa upande wake Mkuu wa wikaya ya Nkasi, Peter Lijuakali amesema ataendelea kuhakikisha watendaji wa halmashauri wanazingatia matumizi sahihi ya fedha za umma na kuhakikisha miradi inakuwa bora.

“Nilifika hapa awali na kubaini matumizi ya Sh milioni 60 kinyume cha utaratibu kwani jengo hilo wanalodai ni OPD, liliianzishwa na wananchi tofauti na fedha zilizotolewa na serikali Sh milioni 500 za sasa hivyo nikaaagiza lisimame,” alisema Lijuakali.

Mkirikiti ameanza ziara ya siku mbili kwenye wilaya ya Nkasi kukagua miradi ya elimu, afya, bandari ya Kabwe. Pia anatarajiwa kuzungumza na wananchi kutoa elimu namna ya kujikinga na maambukizi ya UVIKO-19  kwa kujitokeza kupata chanjo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

THRDC yaongeza mkataba wa ushirikiano na ABA

Spread the love  MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),...

Habari Mchanganyiko

Rufaa ya Equity Benki, State Oil yakwama

Spread the loveMAHAKAMA ya Rufani, jijini Dar es Salaam, imeshindwa kuendelea na...

Habari Mchanganyiko

Bodaboda waeleza mafanikio mafunzo usalama barabarani

Spread the loveMADEREVA bodaboda katika Jiji la Dodoma wameeleza jinsi mafunzo ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yaahidi kuendelea kuunga mkono Serikali za Mitaa

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imesisitiza dhamira yake ya...

error: Content is protected !!