Tuesday , 21 May 2024
Home Kitengo Biashara SBL yazindua programu ya “Learning for Life” kuwajengea uwezo vijana Hanang
Biashara

SBL yazindua programu ya “Learning for Life” kuwajengea uwezo vijana Hanang

Spread the love

 

KAMPUNI ya Serengeti Breweries Limited (SBL) imezindua programu ya “Learning for Life” itakayogusa vijana wa wilaya ya Hanang kwa lengo la kuwapa ujuzi na maarifa muhimu kwa ajili ya maendeleo binafsi, ujasiriamali, usimamizi wa kifedha, na mipango bora ya biashara zao. Anaripoti Mwandishi Wetu, Manyara … (endelea).

Programu hiyo ya SBL itawagusa zaidi ya vijana 400 wa Hanang ambayo leo tarehe 18 Septemba, 2023 na kumalizika tarehe 21 Septemba 2023.

Warsha ya kujifunza kwa maisha inakwenda sambamba kikamilifu na lengo la Wilaya ya Hanang la kutoa huduma bora na zilizo endelevu ifikapo mwaka 2025. Kwa kuwajengea vijana wetu ujuzi muhimu, tunachangia kwenye azma ya wilaya hii ya kuboresha huduma za kijamii na matumizi bora ya rasilimali.

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga, alisema, “Nina furaha kuona Programu ya “Learning for Life” yakifanyika katika Wilaya ya Hanang. Hatua hii ni muhimu sana kwa mkoa wetu na inakwenda sambamba kikamilifu na lengo la Wilaya ya Hanang la kutoa huduma bora na zilzio endelevu ifikapo mwaka 2025.

“Hatua hii haitawawezesha tu vijana wetu bali pia itachangia ukuaji wa kiuchumi na maendeleo ya Wilaya ya Hanang. Itaunda kundi la watu wenye ujuzi na uwezo wa kuleta mabadiliko chanya na uvumbuzi katika jamii yetu.”

Tanzania inajivunia idadi kubwa ya vijana, takriban asilimia 64 ya jumla ya watu, lakini tatizo kubwa la ukosefu wa ajira kwa vijana linaendelea kuwa changamoto, na viwango vya 13.6% kwa vijana wenye umri wa kati ya miaka 15-24.

Upatikanaji mdogo wa mafunzo bora ya ujuzi unachangia tatizo hili, haswa katika Wilaya ya Hanang, ambapo vijana wanafanya karibu asilimia 70 ya idadi ya watu. Ni muhimu kutatua changamoto hii kwa dhati.

Programu ya “Learning for Life” inatoa nafasi ya kuwawezesha vijana kujiajiri na kujenga ajira, lengo kuu la SBL ni kuwasaidia kutambua fursa na kuzitumia kwa ufanisi. Fursa hii inawawezesha vijana kutengeneza mtandao wa kijamii, kujifunza kutoka kwa wataalamu, na kupata ufahamu wa vitendo katika sekta mbalimbali, yote haya yakiwa na lengo la kupunguza ukosefu wa ajira, kupunguza umaskini, na kutengeneza fursa kwa vijana wa Wilaya ya Hanang.

Meneja wa Mawasiliano na Uendelevu wa SBL, Rispa Hatibu

Meneja wa Mawasiliano na Uendelevu wa SBL, Rispa Hatibu alisema: “Serengeti Breweries Limited inaamini kuwa kuwekeza kwa vijana ni kulinda mustakabali wa jamii yetu. Kupitia programu ya Kujifunza kwa Maisha, Serengeti Breweries Limited inatoa ujuzi na pia inakuza uwezo wa vijana wa Hanang kuwa viongozi, wajasiriamali, na wachangiaji katika ukuaji na mafanikio ya wilaya hii.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaElimu

Benki ya Exim yazindua huduma ya ‘Exim Smart Shule’

Spread the love  KATIKA juhudi za kuboresha teknolojia za kidijitali katika sekta...

Biashara

Shinda mkwanja Meridianbet Kasino, ukicheza Expanse Tournament.

Spread the love  LION Kingdom ni sloti kutoka kasino ya mtandaoni yenye...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yapata idhini kuwa wakala wa madalali wa DSE

Spread the loveBenki ya NMB imepata idhini kutoka Benki Kuu ya Tanzania...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Waziri aipongeza NBS kwa mafanikio

Spread the loveNaibu Waziri wa Fedha, Hamad Chande amepongeza Ofisi ya Taifa...

error: Content is protected !!