Saturday , 27 April 2024
Home Kitengo Biashara SBL yazindua ‘Maokoto chini ya Kizibo’ wateja kushinda mpaka Mil. 1.5
Biashara

SBL yazindua ‘Maokoto chini ya Kizibo’ wateja kushinda mpaka Mil. 1.5

Spread the love

 

KAMPUNI ya Bia ya Serengeti Breweries Limited (SBL), imezindua kampeni yake ya ‘Maokoto chini ya Kizibo’ ambayo itawafanya wapenzi wa bia kuwa na kila sababu ya kutabasamu wakielekea benki, kutokana na kampeni kabambe ambayo itatoa zawadi zenye jumla ya kiasi cha Sh. 1.5 bilioni kwa muda wa miezi 3. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Kampeni hiyo itakayowalenga wateja nchni kote, imezinduliwa jana katika ukumbi wa Kitambaa Cheupe Lounge, Sinza jijini Dar es Salaam na inatarajiwa kudumu mpaka mwezi Desemba, 2023. Kampeni hii inatoa fursa kwa kampuni kuwashukuru wateja wake na kuwataka kuendelea kufurahia bidhaa zake.

Kupitia hatua hii, SBL inalenga kuonyesha upendo na shukrani kwa wateja wake waaminifu huku ikiwataka kuendelea kufurahia bia yenye ubora wa hali ya juu. Katika wiki zijazo, SBL inakusudia kuwazawadia wateja wake na ofa za kusisimua, mashindano na zawadi, ikitoa fursa ya kushinda zawadi za kuvutia na kufurahia kumbukumbu za aina yake.

Akizungumza wakati wa uzinduzi, Mkurugenzi Mtendaji na Afisa Mtendaji Mkuu wa East African Breweries Limited (EABL), Jane Karuku amesema, “Tunajivunia kutoa zawadi za kusisimua ambazo sio tu zitaleta furaha lakini pia kutoa frusa ya kujipatia kipato. Zawadi mbalimbali za kifedha zitanufaisha idadi kubwa ya wateja, hatimaye kuwasaidia watu wengi zaidi kuwa na kipato kwa muda mrefu.

Mkurugenzi Mtendaji wa SBL, Obinna Anyalebechi, amesisitiza, “MAOKOTO CHINI YA KIZIBO” inasukumwa na azma ya kuibua hisia za furaha na kusaidia maisha ya wateja wetu, na nia ya kuacha alama muhimu kwa kuleta sababu za kusherekea kila mahali, na kujitolea kwetu kwa namna ya kipekee kusaidia jamii yetu.”

Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa SBL, Anitha Rwehumbiza, ameongezea kuwa kampeni hiyo itafanyika kwa muda wa miezi mitatu wakiwa wameandaa zawadi zenye thamani ya TZS Bilioni 1.5. Amesema, “Tutakuwa tunatoa zawadi za TZS 4M kila wiki na zawadi nyinginezo za papo kwa hapo kila watakapokuwa wananunua bidhaa zetu mbalimbali kama vile Serengeti Premium Lite, Serengeti Premium Lager, Pilsner, Guiness Smooth, na Smirnoff Ice Black”.

William Lyimo, a.k.a. BillNass, mwanamuziki mashuhuri katika Tasnia ya burudani Tanzania na balozi wa kampeni hiyo, amesema, “Nimefurahia dhamira ya SBL katika kuleta furaha na kusaidia maisha ya wateja wake. ‘MAOKOTO CHINI YA KIZIBO’ inaburudisha, hata kwa masharti yake, tayari unaweza kujionea namna ilivyopokelewa vizuri sokoni”.

26 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Biashara

Sloti ya Mega Jade kasino njia 10 za malipo unaposhinda

Spread the love  TUNAKULETEA mchezo wa kasino wa kufurahisha sana ambapo unapewa...

Biashara

Orb of Destiny kutoka Meridianbet kasino ushindi kwa njia 14  

Spread the love  ORB of Destiny ni mchezo wa sloti kutoka kwa...

Biashara

Jiandalie Strawberry Cocktail yako nyumbani huku unacheza kasino 

Spread the love  UTAANDAA matunda yako unayotaka kutumia unaweza kutumia Strawberry, Cantaloupe...

Biashara

420 Blaze It chimbo jipya la kuchota mihela Meridianbet kasino 

Spread the love  JE, umewahi kucheza mchezo wa droo wenye droo 10?...

error: Content is protected !!