Sunday , 28 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Samia: Wanaoharibu kazi serikalini hawatoteuliwa…
Habari za SiasaTangulizi

Samia: Wanaoharibu kazi serikalini hawatoteuliwa…

Spread the love

RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan amesema viongozi wa umma wanaofanya vibaya katika utekelezaji wa majukumu yao, hawatapewa nafasi nyingine serikalini. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Mkuu huyo wa nchi ameyasema hayo jana tarehe 12 Oktoba 2023, Ikulu jijini Dar es Salaam, akipokea ripoti ya kamati aliyounda kutathmini ufanisi na utendaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Alitoa kauli hiyo wakati akizungumzia changamoto za utendaji wa mabalozi wanaoteuliwa kwenda kuiwakilisha nchi katika mataifa mbalimbali.

“Nani akichafua wapi atoke lakini tunampeleka wapi ubalozini. Ukigeuka huku kamanda hapa na wao wana ya kwao, sasa mheshimiwa sisi ukitusaidia huyu na huyu aondoke hapa tutakwenda vizuri zaidi, naletewa. Kwa hiyo najaza huko, sasa hujui nani, hujui nafasi ngapi za kisiasa na ni ngapi za kitaaluma, ndiyo mchanganyiko tulio nao,” alisema Rais Samia.

Alisema kama  “Polisi huko kavuruga IGP mpeleke huko, kwa hiyo lazima tuliangalie hilo vizuri sasa hivi anayevurunda kazini akae pembeni. Tufumbe macho hakuna hili, hakuna lile, hakuna kumpoza akae pembeni asipelekwe popote,”alisema Rais Samia.

Katika hatua nyingine, Rais Samia alisema kuna changamoto ya uhaba wa wataalamu wa mambo ya nje, kitendo kinacholeta changamoto katika teuzi “nafasi za kisiasa hatusemi zisiwepo lakini kwa asilimia ngapi lazima tujipange vizuri na wakati mwingine unajikuta hata hao wanataalamu wa kwenda huko hawapo tunaondoa wizarani amekaa muda mrefu mpeleke.”

Akizungumzia utendaji wa wizara hiyo, Rais Samia alisema inatakiwa kufanyiwa mapitio mara kwa mara ili kuangalia namna ya kuboresha utendaji wake ukidhi siasa za ndani, uhusiano na ushirikiano wa nchi kimataifa, pamoja na kufanya maboresho ya Sera ya Mambo ya Nje ya 2001.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

Habari za Siasa

Sauti ya Watanzania waeleza sababu za kuiunga mkono Chadema

Spread the love  KIKUNDI kinachojipambanua katika kupigania rasilimali na uhuru wa nchi,...

Habari MchanganyikoTangulizi

Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti

Spread the love  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

error: Content is protected !!