Saturday , 4 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Samia awajibu wanaompinga, Nchi haiuziki
Habari za SiasaTangulizi

Samia awajibu wanaompinga, Nchi haiuziki

Spread the love

 

RAIS wa Jamhuri, Samia Suluhu Hassan, ameeleza kuwa nchi haijauzwa na wala haiziki, na kwamba Tanzania ni moja. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza mjini Mwanza juzi, Rais Samia alisema, hakuna mtu au kiongozi ambaye ana nia ya kuuza nchi, bali kinachofanyika ni kutafuta namna bora ya kuendesha serikali na kuhudumia wananchi.

Alisema, “Tanzania ni moja… haigawanyiki wala haiuziki. Kwa hiyo ndugu zangu… Tanzania haiwezi kugawanyika wala kuuzwa. Tunachotafuta ni maendeleo kwa ajili ya watu wote.”

Rais alikuwa akizungumza kwa mara ya kwanza tangu kuibuka mjadala kuhusiana na uamuzi wake wa serikali yake wa kuingiza mkataba katika kuendesha miradi mbalimbali, ukiwamo uendeshaji na usimamizi wa bandari ya Dar es Salaam.

Alisema, uendeshaji umekuwa na maoni mchanganyiko nchini Tanzania baada ya rais Samia Suluhu Hassan kuzungumzia kwa mara ya kwanza sakata la mkataba wa uendeshaji wa bandari akisema.

Kwa muda wiki moja sasa, “nchi imevimba” kufuatia uamuzi wa serikali kutaka kujifunga kwenye mkataba na kampuni moja ya Dubai – Dubai Polrt Wolrd – kuendesha bandari ya Dar es Salaam, ambayo ndio kitovu uchumi wa nchi.

 Kauli ya Rais Samia inalenga kile baadhi ya wachambuzi wa kisiasa wanakiita, ni katika jitihada zake za kutaka kutuliza hali ya mambo.

“Huu ni ujumbe mkubwa kwa wapinzani wake wa kisiasa ndani na nje ya chama chake. Ni wote wenye nia tofauti na yeye, wakiwamo wafanyakazi wa umma,” ameeleza Richard Rwengeza, mkazi wa Mwanza, anayefuatilia ziara ya rais mkoani humo.

Pamoja na serikali kujitokeza mara kwa mara kujaribu kuweka sawa kuhusiana na mkataba huo, bado wasiwasi unaendelea kusalia kwa wananchi wengi na huku baadhi ya wachambuzi wanaongeza kwa kusema kauli ya Rais Samia inadhihirisha namna suala hilo la mikataba ya kigeni linavyoendelea kuwa gumu na tete.

Mkataba kati ya serikali ya Tanzania, tayari umewaibua wanasiasa kadhaa, akiwamo aliyewahi kuwa katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibroad Slaa, ambaye amesema, ikiwa marekebisho hayatafanyika, basi wananchi wanaweza kujitosa mtaani kuandamana.

Dk. Slaa ametoa siku thelathini kwa serikali kushughulikia suala hilo, vinginevyo ametaka wananchi kulipinga kwa njia ya maandamano.

Naye Prof. Ibrahim Lipumba, mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), amedai kuwa ikiwa yaliyomo kwenye mkataba yatabaki kama yalivyo, “hakuna namna ambayo Rais Samia, ataweza kujiondoa kwenye tuhuma na shutuma za muda mrefu, kwamba ameuza nchi na kukabidhi uhuru wake kwa wageni.”

Anasema, baadhi ya vifungu vilivyomo kwenye mkataba wa ushirikiano, vinatilia shaka kuwa mkataba huo, umeandaliwa nchini na umeshirikisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG). Anasema, “yawezekana umeandaliwa Dubai na sisi tumeubeba kama ulivyo.”

Ametolea mfano wa Ibara ya 23 (4) ya mkataba, inayozuia Serikali ya Jamhuri ya Muungano kujiondoa katika mkataba iliyojifunga.

Anasema, “…kifungu hicho kinaeleza mkataba hautavunjwa, hautaondolewa na hautasitishwa, kwa jambo lolote lile. Hata mkivunja uhusiano wa kidiplomalisia, bado mkataba utaendelea kuishi.”

Tayari Bunge la Tanzania limeridhia mkataba huo, hatua ambayo imesababisha ghadhabu kubwa kwa baadhi ya wananchi, wakiwamo viongozi wa madhehebu ya kidini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

Habari za Siasa

Serikali yasaka bilioni 3 kujenga daraja Mto Mpiji

Spread the loveSerikali imesema inaendelea na juhudi za kutafuta fedha kiasi cha...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kwafukuta kisa chaguzi, Lissu aibua tuhuma nzito

Spread the loveCHAGUZI za kusaka viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo...

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga “HIDAYA” chaendelea kuimarika, wananchi wapewa tahadhari

Spread the loveMAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kutoa taarifa...

error: Content is protected !!