Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Samia ataka askari waliopandishwa vyeo kurudi kusimamia wafungwa
Habari za Siasa

Samia ataka askari waliopandishwa vyeo kurudi kusimamia wafungwa

Rais Samia Suluhu Hassan
Spread the love

 

RAIS Samia Suluhu Hassan amesema hatotoa ajira mpya kwa askari wa jeshi la Magereza na kuagiza waliopandishwa vyeo kurudi kusimamia wafungwa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Rais Samia ameyasema hay oleo Ijumaa tarehe 25 Machi 2022 wakati akizundua miradi mbalimbali ya jeshi la Magereza Dodoma.

Amesema kama upandishaji vyeo umesababisha upungufu wa askri wa chini basi inawezekana waliopandishwa wengi hawana kazi za kufanya ofisini, “inawezekana wanazunguka tu kwenye korido za ofisi warudi wakasimamie wafungwa”

“Kusimamia wafungwa kunataka wazoefu. Wale niliowapandisha vyeo ni wazoefu zaidi na warudi wakasimamie wafungwa. Kwa sasa sitatoa ajira. Haina maana kama mtu anapanda cheo anakwenda kukaa ofisini hawana kazi, arudi afanye kazi cheo chako utabaki nacho,” amesema Rais Samia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!