Sunday , 5 February 2023
Home Kitengo Michezo Italia yang’olewa kombe la dunia
Michezo

Italia yang’olewa kombe la dunia

Spread the love

 

MABINGWA wa Ulaya, Italia hawatacheza Kombe la Dunia la mwaka 2022 baada ya kushangazwa na Macedonia Kaskazini katika mechi yao ya mchujo mjini Palermo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Aleksandar Trajkovski alitumia pasi iliyolegea katika dakika ya 92, akasonga mbele na kuachia bao la ushindi kutoka nje ya eneo la hatari.

Bao hilo liliibua shangwe kali kwenye benchi ya Macedonia Kaskazini, huku wachezaji wa Italia na wakufunzi wakipiga magoti mbele ya mashabiki wao wa nyumbani.

Hii inamaanisha kuwa Italia, imeshindwa kufuzu kwa Kombe la Dunia kwa mara ya pili mfululizo, na kuhakikisha Azzurri itastahimili angalau miaka 12 kati ya mechi kwenye kipute hicho muhimu cha kandanda .

Haya yanatokea miezi minane tu tangu kikosi cha Roberto Mancini kusherehekea moja ya ushindi wao mkubwa zaidi – kwa kuwashinda Uingereza katika uwanja wa Wembley na kushinda Euro 2020 baada ya kuchukuliwa kuwa wachezaji wa nje watakaoshiriki dimba hilo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

GGML: Uwanja mpya wa Geita Gold FC kukamilika Mei, 2023

Spread the loveUWANJA wa Magogo unaojengwa na Halmashauri ya Mji wa Geita...

Michezo

Wanafunzi chuo Mwalimu Nyerere wapongezwa kwa ushindi

Spread the love  UONGOZI wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA)...

Michezo

Arsenal waipopoa Manchester United

Spread the loveKLABU ya Arsenal inayoshiriki Ligi Kuu England imewatandika Mashetani Wekundu...

Michezo

Mchezaji Singida apoteza maisha mazoezini

Spread the love  MCHEZAJI na kapteni wa timu ya vijana ya Singida...

error: Content is protected !!