May 25, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Safari ya mwisho ya Hayati Magufuli Chato

Jeneza lililobeba mwili wa aliyekuwa Rais wa Tanzania, John Magufuli

Spread the love

 

MWILI wa aliyekuwa Rais wa Tanzania, Dk. John Pombe Joseph Magufuli unazikwa leo Ijumaa tarehe 26 Machi 2021, katika makaburi ya nyumbani kwao, Chato mkoani Geita.

Viongozi mbalimbali wamehudhulia katika shughuli hiyo ya mwisho ya Hayati Magufuli inaanzisa Uwanja wa Mpira wa Miguu wa Magufuli, wakiongozwa na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Dk. Magufuli, alifariki dunia Jumatano ya tarehe 17 Machi 2021, katika Hospitali ya Mzena, Makumbusho mkoani Dar es Salaam, kwa ugonjwa wa mfumo wa umeme wa moyo.

Baadhi ya viongozi waliopo uwanjani hapo kunakofanyika misa takatifu kukifuatiwa na salamu mbalimbali ni; Marais wastaafu wa Tanzania, Jakaya Kikwete, Ali Hassan Mwinyi.

Wengine ni, Rais mstaafu wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi, Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Othuman Masoud Othuman na Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla na Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa.

error: Content is protected !!