May 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Maaskofu 15, Mapadri 70 wamzika Magufuli

Spread the love

 

MAASKOFU 15 na mapadri zaidi ya 70 wa Kanisa Katoliki, wanashiriki misa takatifu ya kumwombea Hayati John Pombe Joseph Magufuli. Anaripoti Regina Mkonde, Chato …(endelea)

Misa takatifu inafanyika Uwanja wa Mpira wa Magufuli, Chato mkoani Geita leo Ijumaa, tarehe 26 Machi 2021.

Misa hiyo inaongozwa na Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanania (TEC), Gervas Nyaisonga.

Baada ya kumazilika kwa misa hiyo, kutafutia salamu za viongozi mbalimbali akiwemo Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kisha safari ya kwenda makaburi ya familia itaanza ili kuuzika mwili huo.

Misa ya maziko, itaongozwa na Askofu wa Jimbo Katoliki la Rulenge-Ngara, Severine Niwemugizi.

Dk. Magufuli, aliyekuwa Rais wa Tanzania, alifariki dunia Jumatano tarehe 17 Machi 2021, katika Hospitali ya Mzena, Makumbusho mkoani Dar es Salaam.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI TV, MwanaHALISI Online na mitandao yetu kwa habari na taarifa mbalimbali.

error: Content is protected !!