Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Sabaya azidi kung’ang’aniwa
Habari za SiasaTangulizi

Sabaya azidi kung’ang’aniwa

Lengai Ole Sabaya akiwa mahakamani Arusha
Spread the love

 

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Arusha, imeelezwa upelelezi kesi ya jinai ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya (34) na wenzake sita, umekamilika. Anaripoti Mwandishi Wetu, Arusha … (endelea).

Hayo yameelezwa leo Ijumaa tarehe 13 Agosti 2021 na Wakili Mkuu wa Serikali, Tumaini Kweka, mbele ya Hakimu Mkuu Mkazi Martha Mahumbuga na kuomba 27 Agosti 2021, kuruhusiwa kusomewa hoja za awali.

Hakimu Mahumbuga ambaye anasikiliza shauri hilo namba 27/2021 amesema hayo, kufuatia Kweka kuieleza mahakama kuwa upelelezi a shauri hilo umelamilika.

Amesema, “hatua ya upelelezi katika shauri hili umekalimika na kwa sababu ni shauri la uhujumu uchumi, mahakama yenye mamlaka ni mahakama kuu tunaomba tarehe nyingine ili tukamilishe taratibu za kisheria ili mahakamaa yako iweze kuendelea na shauri hili.”

Aidha, Kweka aliwapatia upande wa utetezi hati za mashitaka zilizoongeza washitakiwa kwenye shauri hilo ambalo wanakabiliwa na mashitaka manne tofauti.

Washitakiwa wengine kwenye shauri hilo, ni Enock Mnkeni (41), maarufu Dikdik, Watson Mwahomange (27), maarufu Mamimungu; John Aweyo, maarufu Mike One; Silvester Nyengu (26), maarufu Kicheche, Jackson Macha (29) na Nathan Msuya (31).

Katika shauri upande jamhuri Wakili wa serikali mkuu, Tumain Kweka anashirikiana na mawakili wa serikali, Felix Kwetukia na Baraka Mgaya huku upande wa utetezi ukiwakilishwa na mawakili, Dancan Oola na Mosses Mahuna.

Kweka aliieleza mahakama hiyo kuwa katika shitaka la kwanza, Sabaya anadaiwa kuongoza genge la uhalifu, kinyume cha sheria. Anadaiwa kushirikiana na washitakiwa wengine ambao siyo watumishi wa umma.

Kwamba, tarehe 20 Januari 2021 katika maeneo mbalimbali ya jiji la Arusha, Sabaya akiwa ni ofisa wa umma, mkuu wa wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, alikiuka majukumu yake ya kiofisi kwa pamoja akishirikiana na Mnikeni, Mwahomange, Aweyo na Nyengu.

Kwa kujua na kwa malengo ambayo si halali, kwa kutumia mamlaka yake kama afisa wa umma, Sabaya alijipatia manufaa kinyume cha sheria.

1 Comment

  • Baada ya sabaya kujiona yupo juu ya sheria next bashite & Musiba. Hao walijiona wapo juu ya sheria kwa kujifanya watu wasiojulikana kwa kuwateka watu, kuwaibia,na kuwauwa, allah hazihakiwi analipa hapahapa dunian kila mmoja na hukumu yake aliyoipanga Allah.viongozi mliopo madarakani jifunzeni dunia ni mapito tuuu ukijiona wewe mwamba hakuna wa kukubabaisha ni kujidanganya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!