Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Ruge Mutahaba afariki dunia, Rais Magufuli amlilia
Habari MchanganyikoTangulizi

Ruge Mutahaba afariki dunia, Rais Magufuli amlilia

Spread the love

MKURUGENZI wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba amefariki dunia leo nchini Afrika Kusini alipokuwa akipatiwa matibabu. Anaripoti Khalifa Abdallah … (endelea).

Awali, taarifa za kifo cha Ruge zilianza kujulikana mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli kuandika kupitia ukurasa wake wa mtandao wa twitter kuwa amepata taarifa ya kifo hicho.

“Nimepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha kijana wangu Ruge Mutahaba. Daima nitamkumbuka kwa mchango wake mkubwa ktk tasnia ya habari, burudani, na juhudi za kujenga fikra za maendeleo kwa vijana. Poleni wanafamilia,ndugu,jamaa na marafiki. Mungu amweke mahali pema, Amina,” aliandika Rais Magufuli kupitia ukurasa wake rasmi wa Twitter.

Hadi umauti unamfika, Ruge alikuwa nchini Afrika Kusini akipatiwa matibabu ambapo alikuwa akisumbuliwa na tatizo la Figo, aliugua kwa zaidi ya miezi minne akaanza kupatiwa matibu Dar es Salaam katika hospitali ya Kairuki, akapelekwa India na baadae Afrika Kusini ambapo ndipo umauti ulipomkuta.

MwanaHALISI ONLINE itakujuza zaidi. Pumzika kwa amani Ruge Mutahaba.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

error: Content is protected !!