Saturday , 3 June 2023
Home Habari Mchanganyiko Baada ya miezi minane mochwali, mwili kuzikwa wiki hii
Habari Mchanganyiko

Baada ya miezi minane mochwali, mwili kuzikwa wiki hii

Spread the love

FAMILIA ya marehemu Frank Kapange imeamua kuchukua mwili wa kijana wao uliohifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya kwa zaidi ya miezi minane ili kufanya taratibu za mazishi wiki hii. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Familia hiyo iligoma kuchukua mwili wa Frank kwa ajili ya mazishi wakitaka uchunguzi ufanyike kuhusu chanzo cha kifo hicho kilichotokea tarehe 4 Juni 2018 ufanyike.

Familia ya Frank ilifungua shauri katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya wakiiomba mahakama kutoa amri ya kufanyiika kwa uchunguzi wa kifo cha kijana wao, lakini shauri hilo lilitupiliwa mbali. Kutokana na familia hiyo kutoridhika na uamuzi huo, walikata rufaa katika Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya ambayo pia iliifuta kesi hiyo baada ya kujiridhisha kwamba mlalamikaji hakufuata taratibu wakati wa kuifungua kesi hiyo.

Msemaji wa Familia ya Frank, Julius Kapange amesema wameuchukua mwili huo kwa ajili ya kufanya mazishi huku akiitupia lawama mahakama kwa kutotoa kibali cha kufanyika kwa uchunguzi wa kifo cha kijana wao.

“Kama familia imetusumbua sana siwezi kuendelea zaidi, ila nasikitika kwa sababu haki haijatendeka sababu lengo letu ilikuwa si kushindana na serikali, tulitegemea mahakama itatupa kibali cha kusema huyu marehemu amekufa kwa njia hii, angefanyiwa vipimo wakishapima watukabidhi mwili kwa amani tukazike, vipimo hatujapewa niliitwa tu nitambue maiti kama ni yangu nikatambua ni kijana wangu, “ amesema Kapange.

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Mbeya, Dk. Godlove Mbwanji leo tarehe 26 Februari 2019  amesema  hospitali hiyo imesamehe gharama za kuhifadhia maiti katika kipindi hicho cha miezi nane na kwamba familia hiyo iko huru kufanya mazishi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Magunia 731 ya bangi yakamatwa, mamia ya hekari yateketezwa Arumeru

Spread the love  MAMIA ya magunia ya madawa ya kulevya aina ya...

Habari MchanganyikoTangulizi

Bosi NIC apandishwa kizimbani, akabiliwa na mashitaka 365

Spread the love  ALIYEKUWA Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bima la Taifa...

Habari Mchanganyiko

Serikali yakabidhi eneo la mahakama ya Afrika ya haki za binadamu

Spread the loveSerikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa...

Habari Mchanganyiko

Udhamini wa NMB mikutano ya ALAT wafikia 1.2 bilioni

Spread the loveBENKI ya NMB imeendelea kufanya kazi kwa karibu na Asasi...

error: Content is protected !!