Tuesday , 27 February 2024
Home Kitengo Michezo Rekodi ya 1977 inayosakwa na wachezaji Simba, Yanga
Michezo

Rekodi ya 1977 inayosakwa na wachezaji Simba, Yanga

Spread the love

 

WACHEZAJI wa kabu kubwa Tanzania – Simba na Yanga zote za jijini Dar es Salaam, wana jambo ambalo hawajaweza kulifanya tangu lilipofanyika mwaka 1977. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Jambo hilo ni rekodi ya hat-trick iliyofanywa na mchezaji wa zamani wa Simba, Abdallah Kibadeni ‘King Kibaden’ tarehe 19 Julai 1977, dhidi ya hasimu wao Yanga.

Katika mchezo huo, Kibadeni aliifunga Yanga bao tatu kuanzia dakika ya za 10, 42 na 89 ambapo mchezo huo ulimalizika kwa Yanga kufungwa bao 6-0.

Selemani Matola, Kocha Msaidizi wa Simba

Magoli mengine yalifungwa na Suleiman Sanga, beki wa Yanga aliyejifungwa mwenyewe ambapo magoli mawili yalifungwa na Jumanne Hassan.

Tangu mwaka huo, hakuna mchezaji yeyote aliyewahi kufunga bao tatu katika mechi zinazokutanisha watani hao wa jadi.

Mpaka sasa, rekodi zinaonesha Simba na Yanga zimekutana mara 105, ambapo Yanga ameshinda mara 37, Simba 31 sare zikiwa 37.

Kocha Mkuu wa Yanga, Nadreddine Al Nabi

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Wizara yaahidi kuboresha, kuimarisha michezo

Spread the loveIkiwa ni saa kadhaa baada ya kumalizika kwa mashindano ya...

Habari MchanganyikoMichezo

Nje jogging yanyakua medali 20 Kili Marathon

Spread the loveTimu ya riadha ya Wizara ya Mambo ya Nje na...

Michezo

Siku ya kukusanya maokoto ni leo, usipange kukosa

Spread the love  HATIMAYE Jumamosi imefika ndugu mteja wa Meridianbet na mechi...

Michezo

Kuwa milionea na Meridianbet ni rahisi sana

Spread the love  JE, unajua kuwa leo hii ni siku nzuri kwako...

error: Content is protected !!