Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko RC Shigela awaonya maofisa ugani wasiokuwa na mashamba darasa
Habari Mchanganyiko

RC Shigela awaonya maofisa ugani wasiokuwa na mashamba darasa

Spread the love

 

MKUU wa mkoa wa Morogoro, Martin Shigela amewata maofisa ugani kutumia taaluma yao kivitendo kwa kuweka mashamba darasa na kuwapa elimu wakulima itakayoleta tija ya kilimo katika maeneo yao. Anaripoti Christina Haule, Morogoro … (endelea).

Hayo yalisemwa na Mkuu wa wilaya ya Malinyi, Mathayo Masele k,wa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Morogoro, wakati akizindua kituo mahili cha usambazaji wa teknolojia za kisasa za kilimo mkoani humo, kilichoandaliwa na Taasisi ya utafiti wa Kilimo nchini (TARI) kikiwa na wataalamu wa mafunzo kwa wakulima  ili kuongeza tija na uzalishaji.

Masele alisema zipo wilaya nyingi ambazo zina maafisa ugani ambao wakiulizwa kazi wanazofanya na kutakiwa kuonesha mashamba darasa yao yalipo hukosa vya kujieleza.

“Kama kuna Afisa ugani anajijua hana shamba darasa na bado anaipenda kazi yake, abadilike mara moja” alisema.

 

Akizungumza kwenye uzinduzi wa kituo hicho mkurugenzi Mkuu wa TARI, Dk. Geofrey Mkamilo alisema kituo hicho kitakachotoa mafunzo mwaka mzima kitakuwa na wataalamu mbalimbali wa kilimo wakiwemo watafiti na wataalamu wa huduma za ugani watakaotoa elimu ya mazao mbalinbali kwa wakulima.

Dk. Mkamilo alisema TARI iko tayari kuhakikisha inaleta mapinduzi ya kilimo na kuhamasisha wakulima kuachana na kilimo mazoea walichokuwa wanalima mababu na mabibi.

Alisema katika kuboresha kilimo na kuongeza uzalishaji nchini TARI imekuwa ikifanya kazi na taasisi nyingine ikiwemo taasisi ya udhibiti wa ubora wa mbegu TOSCI, wakala wa mbegu ASA, na makampuni mengine ya uzalishaji na usambaza mbegu ili kumfanya mkulima kupata elimu ya kilimo na kujua mbegu zinapatikana wapi.

Dk. Mkamilo alisema TARI inaratibu shughuli za utafiti na kuhamasisha matumizi ya teknolojia za kilimo na ubunifu kwa lengo la kuongeza tija ya kilimo nchini.

Naye Mkurugenzi wa kituo cha utafiti TARI Mlingano-Tanga, Dk. Catherine Senkolo aliwashauri wakulima wa migomba kulima mazao ya mikundekumbe kwenye shamba la migomba ili kutunza unyevunyevu na pia kutengeneza mbolea ya samadi.

Dk. Senkolo alisema mikundekunde kwenye shamba la migomba pia linasaidia kuondoa ugonjwa wa minyoo kwenye migomba ambao umekuwa ukisababisha uzalishaji kupungua.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!