Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko RC Mongela awataka wafanyabiashara kuunga mkono kampeni ya GGML Kili Challenge
Habari Mchanganyiko

RC Mongela awataka wafanyabiashara kuunga mkono kampeni ya GGML Kili Challenge

Spread the love
KATIKA kuendeleza mapambano dhidi ya Virusi Vya Ukimwi/ Ukimwi, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongela ametoa wito kwa wafanyabiashara wa mkoa huo na Watanzania kwa ujumla kuchangia fedha katika Kampeni ya GGML Kili Challenge ainayolenga kukusanya fedha kwa ajili ya kutunisha mfuko wa udhamini wa kudhibiti Ukimwi (ATF) pamoja na taasisi binafsi zinazojihusisha kudhibiti janga hilo. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).
Mongela ametoa wito huo tarehe 14 Mei mwaka huu jijini Arusha katika harambee ya kuchangia Kampeni ya Kili challenge 2023 ambayo inaratibiwa na Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) kwa kushirikiana na Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS).
Makamu Rais wa AngloGold Ashanti- GGML anayeshughulikia miradi endelevu, Simon Shayo (katikati) akimpatia zawadi Mkuu wa mkoa Arusha, John Mongela. Kulia ni Mkurugenzi mtendaji wa TACAIDS, Dk. Leonard Maboko.
Amesema kampeni hiyo iliyoasisiwa na GGML mwaka 2002, imekuwa mstari wa mbele katika kuunga mkono juhudi za Serikali kuendeleza mapambano dhidi ya VVU na Ukimwi.
“Fedha hizi zitasaidia wenye uhitaji na baadhi ya fedha zinazopatikana zitawekwa kwenye Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti UKIMWI (ATF) kwa ajili ya mwitikio wa UKIMWI nchini,” amesema.
Aidha, Makamu Rais wa Anglo Gold Ashanti- GGML anayeshughulikia miradi endelevu kwa upande wa Ghana na Tanzania, Simon Shayo amesema kampeni hiyo mwaka huu inatarajiwa kukusanya dola za Marekani milioni moja sawa na Sh bilioni 2.3.
“Fedha hizo ambazo hukusanywa kila mwaka, hulenga kuchangia juhudi za serikali ya Tanzania katika jitihada zake kufikia malengo ya sifuri tatu yaani kupunguza kabisa kwa kufikia asilimia sifuri ya maambukizi mapya, sifuri ya unyanyapaa pamoja na sifuri katika vifo vitokanavyo na UKIMWI,” amesema na kuongeza kuwa;
“GGML imepokea msaada ambao uliiwezesha Kili Challenge kupiga hatua kubwa hadi kufikia kuwa mfuko wa kimataifa, wenye kushirikisha wapanda mlima na waendesha baiskeli kutoka mabara yote na zaidi ya nchi 20.
Amesema mwaka huu wamekuja tena kuendeleza mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI, hivyo GGM kwa kushirikiana na Tume ya Kudhibiti Ukimwi nchini (TACAIDS) tunawakaribisha sana wadau wetu na makampuni mbalimbali kuchangia na kushiriki kampeni hii.
Kurugenzi Mtendaji wa TACAIDS Dk. Leonard Maboko naye ametoa wito kwa Watanzania kuungana na serikali katika kutunisha fedha za mfuko huo wa ATF ihasa ikizingatiwa utegemezi kutoka kwa wahisani katika kipindi cha karibuni umepungua kwa kiasi kikubwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mvungi aendesha kikao kazi cha wataalam wa Regrow

Spread the love  MKURUGENZI wa Idara Sera na Mipango Wizara ya Maliasili...

Habari MchanganyikoTangulizi

Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti

Spread the love  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,...

Habari Mchanganyiko

Polisi wakanusha kufanya uzembe ajali iliyouwa mwandishi Ayo Tv

Spread the loveJESHI la Polisi limekanusha tuhuma zilizoibuliwa dhidi yake  kwamba limekawia...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia kuzindua gazeti litakalotoa habari za wafanyakazi Tanzania

Spread the loveSHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), liko mbioni kufufua...

error: Content is protected !!