Saturday , 13 April 2024
Home Habari Mchanganyiko RC Dodoma ataka uwekezaji wenye tija
Habari Mchanganyiko

RC Dodoma ataka uwekezaji wenye tija

Spread the love

MKUU wa Mkoa wa Dodoma Dk. Binilith Mahenge amesema kuwa ili kuwa na jiji lenye maendeleo ya haraka ni lazima wawekezaji wawekeze kwenye miradi yenye manufaa kwa jamii na kwa taifa. Anaripoti Dany Tibason … (endelea).

Mbali na hilo mkuu huyo aliwataka wawekezaji kuhakikisha wanawekeza kwenye miradi ambayo inaliongezea taifa kipato kutokana na kulipa kodi kwa uhaminifu na kuepukana na kukwepa kulipa kodi ambazo zipo kisheria.

Dk. Mahenge alitoa kauli leo jijini hapa alipokuwa akizindua mfumo wa ukataji wa tiketi za kielektroniki kwa kampuni ya mabasi ya ABC.

Dk. Mahenge amesema kuwa uwekezaji ambao unaendana na teknolojia kwa kulipa malipo mbalimbali utapunguza upotezu wa pato la taifa na kumfanya mwekezaji kuwa na kumbukumbu muhimu za makusanyo yake pasipokuwepo na udanganyifu.

Aidha amesema kuwa matumizi ya teknolojia za kisasa itasaidia wanadodoma kupata huduma kwa urahisi na kuondokana na changamoto ya kutumia muda mwingi kufuata huduma.

Akizungumza na wananchi pamoja na abiria waliokuwa wapo katika kituo hicho Dk. Mahenge amesema wanadodoma wanatakiwa tutumie fursa za kisasa ili kubana matumizi ya muda kwa kupata huduma mahali ulipo badala ya kutumia muda mwingi kufuata huduma mbali.

Alieleza kuwa serikali imejipanga kuhakikisha jiji hilo linakuwa tofauti na majiji mengine kwenye upatikanaji wa huduma na ujenzi wa miundombinu.

“Tunataka tuwe na jiji linalovutia kwa kuwekewa miundombinu na uboreshaji wa huduma mbalimbali, hichi kilichofanywa na kampuni hii ni kuunga mkono jitihada za Rais John Magufuli za Dodoma za kuifanya Dodoma kuwa Makao makuu ya nchi,” amesema.

Amesema pia lengo la Rais ni kuhakikisha kunakuwa na makao makuu yenye huduma nzuri za usafirishaji, miundombinu bora ya barabara na reli hivyo kukuza uchumi wa nchi kutokana na ukusanyaji mzuri wa mapato.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Severine Ngallo amesema kampuni hiyo imeamua kuanzisha mfumo huo ili kurahisisha utoaji huduma na usalama wa abiria.

Amesema kampuni imeamua kuanzisha huduma hiyo ili kuwaondolea wateja changamoto za kulanguliwa tiketi na kupewa tiketi feki.

“Abiria atatumia simu yake ya mkononi kukata tiketi bila kukutana na wakala yeyote na hatua hii pia itasaidia serikali kupata mapato yake stahiki na kukadiria ulipaji kodi kulingana na kipato cha kampuni,” amesema Ngallo.

Naye, Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi amesema serikali imetenga zaidi ya Sh. 78 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali ikiwemo Kituo kikubwa cha mabasi yaendayo mikoani ambacho kitakuwa kikubwa Afrika mashariki.

3 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Askofu ataka mafisadi, wauza mihadarati washughulikiwe kumuenzi Sokoine

Spread the love  MHASHAMU Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Arusha, Isaac...

Habari MchanganyikoTangulizi

Mafuriko yaua 33 Morogoro, Pwani

Spread the love  SERIKALI ya Tanzania imetoa tathmini ya athari ya mafuriko...

Habari Mchanganyiko

Wanafunzi 7 wahofiwa kufariki gari la shule likitumbukia korongoni

Spread the love  WANAFUNZI saba wanahofiwa kupoteza maisha, huku watatu wakinusurika katika...

Habari Mchanganyiko

Wazazi, walezi watakiwa kuwa karibu na watoto wao

Spread the love  WAZAZI na walezi wameagizwa kuwalea watoto wao katika maadili...

error: Content is protected !!