Friday , 3 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Rais Samia: Tunawagonjwa wa corona zaidi 100
Habari MchanganyikoTangulizi

Rais Samia: Tunawagonjwa wa corona zaidi 100

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema, zaidi ya wagonjwa 100 wa maambukizi corona (COVID-19), wamebainika nchini humo na wanaendelea na matibabu. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Amesema, kati ya wagonjwa 70 wanaendelea na matibabu ya gesi ili kuhakikisha wanapona.

Rais Samia amesema hayo leo Jumatatu, tarehe 28 Juni 2021, Ikulu ya Dar es Salaam, wakati akizungumza na wahariri na waandishi wa habari, kuhusu siku 100 za utawala wake tangu alipoingia madarakani.

Alikuwa akijibu swali aliloulizwa juu ya mikakati ya makusudi ya kupambana na ugonjwa huo.

“Nilipoingia madarakani nilitamani tushughulike na corona kama inavyoshughulikiwa duniani. Niliunda kamati ya wataalamu, wakafanya na kuleta ripoti na tumeamua kwenda kama dunia inavyokwenda.”

“Mpaka juzi Tanzania kuna wagonjwa wa corona kama miamoja na, na kati yao 70 wako kwenye matibabu ya gesi kama takwimu za juzi. Tunapaswa kujikinga wasiongezeke,” amesema Rais Samia

Kuhusu chanjo, Rais Samia amesema “chanjo ya corona itakuja Tanzania lakini itakuwa hiari kwa mtu kuchanjwa, haitakuwa lazima.”

Ameendelea kuwasisitiza wananchi kuchukua tahadhari ya maambukizi hayo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Kasilda Mgeni anasisitiza umoja, ushirikiano Same 

Spread the love  MKUU mpya wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda...

Habari MchanganyikoTangulizi

Hii hapa kauli ya Sheikh mpya mkoa wa Dar

Spread the loveSAA chache baada ya kuteuliwa kukaimu nafasi ya aliyekuwa Sheikh...

Habari MchanganyikoTangulizi

Breaking news! Mufti amng’oa Sheikh mkoa Dar

Spread the loveBARAZA la Ulamaa la Bakwata katika kikao kilichofanyika tarehe 1...

Habari Mchanganyiko

Bilioni 120 za DMDP zaibadilisha Ilala, wananchi watoa ya moyoni

Spread the loveJUMLA ya Sh bilioni 120.7 zimetumiwa na Halmshauri ya Jiji...

error: Content is protected !!