May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia: Mawio, MwanaHALISI, Mseto yapewe leseni

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amesema magazeti yote yaliyofungiwa na kumaliza adhabu zao, wapewe leseni ili waendelee na majukumu yao. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Magazeti yaliyofungiwa na kumaliza adhabu zao zaidi ya mwaka sasa ni; MwanaHALISI, Mawio na Mseto. Pia, Tanzania Daima limenyang’anywa leseni yao.

Rais Samia ametoa agizo hilo leo Jumatatu, tarehe 28 Juni 2021, wakati akijibu swali la Joyce Shebe, Mhariri Mkuu wa Clouds Media.

Ni katika mazungumzo baina ya Rais Samia na wahariri na waandishi wa habari kuhusu siku 100 za utawala wake, tangu alipoingia madarakani tarehe 19 Machi 2021.

“Vyombo vya habari vilivyofungiwa, uliagiza vifunguliwe lakini mpaka sasa havijafunguliwa.”

“Lakini mheshimiwa Rais, adhabu iliyotolewa kwa magazeti haya imekwisha kumalizika ila bado havijafunguliwa, tunaomba Rais uvifungulie,” ameuliza Joyce

Akijibu swali hilo, Rais Samia amesema “waziri yupo amesikia lakini najua kuna magazeti yamekwisha maliza adhabu zao, waende ku process leseni na hawaja process.”

“Kama hawaja process waende wapewe leseni waendelee na kazi zao ila sheria za nchi zifuate,” amesema Rais Samia

error: Content is protected !!