Friday , 3 February 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia: Mimi ni chui jike
Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia: Mimi ni chui jike

Spread the love

 

LICHA ya kukaribishwa na wimbo wa simba jike katika uzinduzi wa Tamasha la utamaduni mkoa Kilimanjaro, Rais Samia Suluhu Hassan amesema yeye ni chui jike. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Rais Samia ametoa kauli hiyo leo Jumamosi tarehe 22 Januari, 2022 katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika (MoCU) wakati akizindua Tamasha la utamaduni mkoa Kilimanjaro, ambalo pia alikuwa mgeni rasmi.

“Leo nimekuja Kilimanjaro kwa ajili ya tamasha la utamaduni, nashukuru nimepata mapokezi mazuri kwenye tamasha hili, nimetunukiwa vazi hili, lakini hapa waimbaji nyimbo walisema mimi ni simba jike lakini kwa vazi hili kumbe ni chui jike.

“Kwa hiyo nashukuru kwa vazi hili la kimila lakini inanipa faraja kwamba kuna chui dume Chifu Mareale naye amevaa vazi hilohilo. Nashukuru kwa zawadi kubwa mliyonipatia wana Kilimanjaro asanteni sana,” amesema Rais Samia.

Pamoja na mambo mengine amesema serikali itaendelea kushirikiana na viongozi wa kimila ikiwemo machifu watemi kama nguzo muhimu ya kuifadhi mila na desturi zetu.

“Hapa nataka nirudie kwa sababu kumekuwa na maneno mengi ndani ya Tanzania… kuhusu uchifu na Serikali kushirikiana na uchifu.

“Nataka niseme tumeamua kuwa na jukwaa la pamoja baina ya serikali, machifu na wazee wa kimila kama nguzo muhimu tushirikiane katika kuhifadhi mila na desturi zetu na katika kuhifadhi maeneo mbalimbali yaliyotunzwa kama njia ya kuhifadhi mazingira ndani ya nchi yetu.

“Maeneo haya yako chini yenu machifu na kwa kutumia njia zenu mbalimbali mmeweza kuzuia wananchi kutokuyavamia maeneo yale kwa mila na desturi zetu mbalimbali,” amesema.

Amesema Serikali itaendelea kushirikiana nao kutunza maeneo hayo na hata yale ambayo yamevamiwa anajua wakiwaweka machifu mbele kwenye kuyahifadhi watafanikiwa katika lengo hilo.

“Tuwashukuru sana machifu kwa utayari huo wa kufanya kazi na serikali. Tutashirikiana katika malengo yenu mliyojiwekea yanayokubali kisheria kama mlivyoeleza katika risala yenu.

“Kwa mtazamo huu mpya tutaendelea kuimarisha bajeti ya wizara ya utamaduni, sanaa na michezo ili iweze kuwa na uwezo zaidi wa kushirikiana nanyi katika kubaini kulinda na kuzitangaza, mila na desturi zetu,” amesema.

1 Comment

 • Mama umesema kweli!
  Ungekubali kuwa Simba Jike, basi Simba Dume ni Raisi wa Kenya. Nakupongeza kwa ujasiri huo. Chui hawana kiongozi….wote ni viongozi!
  Sasa madini yetu yarejeshwe kwetu au wote wanaochimba waingizwe DSE watanzania wanunue hisa za kampuni za madini yetu.
  Wameshakaa TZ zaidi ya miaka mitatu, kwa nini tunaogopa kufuata sheria za “Initial Public Offering” (IPO)?
  Pia weka wazi muda wa mikataba iingizwe kwenye Katiba miaka mitano. Asiyetaka aachie. Miaka 30 na kuendelea tunaibiwa sana. Tufupishe muda tuweze kukomesha uwizi wakiiba.
  Namsubiri Chui Jike, mpole, lakini anashtukiza na kushambulia wezi wa rasilimali zetu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yaiangukia Serikali kunusuru wananchi Liwale, Nachingwea

Spread the love  CHAMA cha ACT-Wazalendo, kimeitaka Serikali kuchukua hatua za haraka...

Habari za SiasaTangulizi

Vigogo wanaokwamisha mradi Liganga na Mchuchuma kitanzani

Spread the love  NAIBU Spika wa Bunge, Mussa Zungu, watu wanaokwamisha utekelezaji...

Habari za Siasa

Gridi ya Taifa kufumuliwa kukabiliana na katizo la mgao wa umeme

Spread the love  WAZIRI wa Nishati, Januari Makamba, amesema Serikali ina mpango...

Habari MchanganyikoTangulizi

Hii hapa kauli ya Sheikh mpya mkoa wa Dar

Spread the loveSAA chache baada ya kuteuliwa kukaimu nafasi ya aliyekuwa Sheikh...

error: Content is protected !!