Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Rais Samia awatoa hofu wanaohoji uamuzi wa kuwarejesha shule waliopata ujauzito
Habari Mchanganyiko

Rais Samia awatoa hofu wanaohoji uamuzi wa kuwarejesha shule waliopata ujauzito

Spread the love

 

RAIS Samia Suluhu Hassan amesema Serikali imeamua kuwarejesha shule watoto wote walioacha shule kwa sababu mbalimbali kama vile, utoro, sababu za kisheria ikiwamo ujauzito, waliofeli darasa la saba kwa bahati mbaya, ili kuwapa fursa watoto wote wa Kitanzania kuendelea na elimu. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea)

Pia amewatoa mashaka watanzania kuhusu uamuzi huo kwamba serikali iko makini hivyo hakutatokea uharibifu wowote ndani ya sekta ya elimu au mfumo wetu wa elimu kuanzia shule ya msingi hadi sekondari.

Rais Samia ametoa kauli hiyo leo tarehe 29 Novemba, 2021 wilayani Chato mkoani Geita katika hafla ya uzinduzi wa Shule ya Msingi na Awali ya Museveni.

Shule hiyo iliyojengwa kwa ufadhili wa Rais wa Uganda, Yoweri Museveni imezinduliwa rasmi na rais huyo aliyekuwepo nchini kwa ziara ya siku tatu.

Aidha, akizungumzia suala hilo la wanafunzi walioachishwa masomo kwa sababu mbalimbali, Rais Samia amesema ameamua kulitoa ufafanuzi suala hilo baada ya kuona mjadala mbalimbali miongoni mwa Watanzania.

“Nataka nitilie mkazo alilosema waziri wa elimu kwamba tumeamua watoto wote ambao wameacha shule kwa sababu mbalimbali, utoro, sababu za kisheria kwamba ukipata mimba huruhusiwi kuendelea na masomo, wale waliodondoka la saba tunajua kuna wanafunzi wetu wazuri sana kwa bahati mbaya wakati wa mtihani hawakufanya vizuri lakini baada ya kukaa nje wamejutia tunawapa nafasi nyingine kurudi na kufanya mitihani.

“Lengo la maamuzi haya ni kutoa fursa pana kwa watoto wa kitanzania kuendelea na elimu. Yanayozungumzwa na watanzania ni pamoja tu watoto waliopata mimba kurudi, kuna wale waliofurahia lakini kuna wale ambao hawakufurahia,” amesema.

Amesema kwa kawaida mtoto wa kike akishakuwa mama kama alikuwa darasa la sita, hatarudi tena darasa la sita kuendelea na shule.

Amesema wale waliopata mimba wakiwa sekondari wanarudi, tena wapo wanaoendelea na masomo yao vizuri na kufika hadi chuo kikuu.

“Kwa hiyo hapa ni suala la kutoa fursa na wenyewe watajipanga lakini kwa wale ambao wanahisi hawataweza kurudia tena shule ya msingi, tumewawekea mkondo mwingine unaitwa elimu mbadala.

“Watakaokwenda kwenye mkondo huo waendelee na masomo yao, tuwafundishe namna ya kujiingiza kwenye miradi ili akitoka hapo aweze kwenda kufanya miradi kujitunza yeye na mtoto aliyemzaa.

“Kwa hiyo hili Watanzania lisitupe wasiwasi na kuchukua muda mrefu kulijadili kwanini mtoto aliyepata ujauzito arudi tena shule, si kawaida kurudi,” amesema.

Ametolea mfano kuwa zipo nchi nyingi zinazofanya hivyo ikiwamo Zanzibar.

“Kwa hiyo yale mashaka ambayo tuliyonayo, niwahakikishie tuko makini tutayashughulikia na hayataleta uharibifu wowote ndani ya sekta ya elimu au mfumo wetu wa elimu, kutoka primary hadi secondary.

“Nimeona nilisemee vizuri hilo kwa sababu tayari nianza kusikia a mijadala kwa hiyo wale wanaolijadili walijadili kwa misingi hiyo. Fursa hii imetoka kwa watoto wote,” ameema.

Kauli ya Rais Samia imekuja siku tano baada ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako ambapo Novemba 24 mwaka huu alitangaza rasmi kuwaruhusu wanafunzi waliokatiza masomo yao kwa kwasababu ya kupata ujauzito wakiwa shuleni kurejea masomoni kupitia mfumo rasmi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma kuhusu mafanikio ya wizara hiyo katika miaka 60 ya uhuru wa Taifa alisema;

“Utaratibu ulivyo sasa mwanafunzi anapofutiwa mtihani wake wa darasa la saba au ambao watafaulu kufeli mtihani wa darasa la saba au anapokuwa amepata tatizo lolote wakati wa mtihani wa darasa la saba atakuwa hana fursa nyingine, sasa tumeamua wanafunzi wanaofeli, kufanya udanganyifu au utovu wa nidhamu watapewa fursa ya kurudia mitihani na watapewa fursa ya kujiunga na shule za sekondari,” alisema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!