Sunday , 29 January 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Shule ya Museveni kusajili wanafunzi 630, Serikali kujenga mabweni, barabara
Habari za Siasa

Shule ya Museveni kusajili wanafunzi 630, Serikali kujenga mabweni, barabara

Spread the love

RAIS Samia Suluhu Hassan amesema katika kutimiza malengo ya Hayati Rais Dk. John Magufuli, Serikali itajenga mabweni, kuongeza nyumba za walimu, barabara na mazingira mazuri ya Shule ya msingi na Awali Museveni iliyopo Chato mkoani Geita. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Rais Samia ametoa kauli hiyo leo tarehe 29 Novemba, 2021 wilayani Chato mkoani Geita katika hafla ya uzinduzi wa Shule ya Msingi na Awali ya Museveni.

Shule hiyo iliyojengwa kwa ufadhili wa Rais wa Uganda, Yoweri Museveni imezinduliwa rasmi na rais huyo aliyekuwepo nchini kwa ziara ya siku tatu.

Amesema Serikali itabeba pale palipobaki ili shule hiyo ifikie viwango ambavyo Hayati Dk. Magufuli  alivyotarajia vifikiwe.

“Wizara ya elimu sayansi na teknolojia kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa (Tamisemi) itaandaa utaratibu wa kuhakikisha uwepo watumishi, vitabu, vifaa muhimu na fedha za uendesha ili shule hii iweze kupokea wananfunzi ifikapo tarehe 15 Januari, 2022,” amesema.

Pia amesema katika kuenzi mchango wa Rais Museveni, wizara ya elimu iweke historia ya Rais Museveni pamoja na Dk. Magufuli katika maktaba iliyopo shuleni hapo.

“Ninaagiza hivyo ili watoto wetu watakaosoma hapa wajue chanzo cha shule hii lakini waelewe historia ya viongozi wetu wawili waliodhamiria na kutimiza ujenzi wa shule hii.

“Lakini pia waelewe falsafa za viongozi wetu za uzalendo, umajumui na falsafa za Rais Museveni katika kuhakikishas waafrika wanajitegemea kwenye sekta za kiuchumi, kijamii na kisiasa,” amesema.

Pia amemuomba Rais Museveni kwamba shule hiyo ya Mseveni ipate shule dada au kaka kule Uganda ili wanafunzi wapate uzoefu na kutembeleana.

Pamoja na mambo mengine amemshukuru Rais Museveni kwa niaba ya Hayati Rais Magufuli kwa utu wema wa kujitoa kwake kuhakikisha kuwa suala la kuwa na elimu bora sio suala la mipaka ila ni jukumu la viongozi wote wa Afrika kuhakikisha Afrika inatoa elimu bora na yenye viwango ili kuweza kukidhi soko la ajira.

“Kuwa na miundombinu ya elimu kama majengo ni hatua moja ila kuwa na mitaala inayokidhi soko la ajira ni kitu kingine,’ amesema.

Amesema shule hiyo itakuwa na manufaa mengi ikiwamo kuongeza fursa kwa wanafunzi wote kupata elimu kwani majengo ya shule hiyo yamezingatia mahitaji ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu.

“Pili itaimarisha utoaji wa elimu bora kwa uwepo wa miundombinu bora yote muhimu. Kwa niaba ya serikali ya Tanzania nikuhakikishie kuwa majengo na miundombinu ya shule hii yatatumika na kutunzwa vizuri ili yaweze kunufaisha watoto wa kitanzania,” amesema.

Kwa upande wake Rais Museveni mbali na kutoa historia ya uamuzi wake wa kujenga shule hiyo, pia alisema zipo shule nyingine mbili ambazo alizijenga hapa nchini kwa lengo la kuenzi mapito aliyopitia wakati akipigana vita vya msituni.

Awali akitoa taarifa kuhusu shule hiyo, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amesema Shule ya awali na Msingi Museveni iliyopo katika kijiji cha Nyabirezi wilayani Chato mkoani Geita ilianza kujengwa tarehe 11 Februari mwaka 2020 na kukamilika Februari mwaka huu.

Amesema shule hiyo itakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 630.

Amesema shule hiyo imesajiliwa kama shule ya kutwa na inatarajiwa kutumia mtaala wa kiingereza (English medium).

“Majengo yaliyojengwa na kukamilika katika shule hii ni jengo la utawala moja, vyumba vya madarasa ya shule ya msingi 17 na maktaba moja, Vyumba vya madarasa ya shule ya elimu ya awali matatu, ofisi kwa ajili ya elimu ya awali mbili, matundu ya vyoo 37 na nyumba ya walimu yenye uwezo wa kuweka familia mbili,” amesema.

Wakati Mkuu wa Mkoa wa Geita, Rosemary Senyamule amesema mkoa huo una shule za msingi 701 kati ya hizo 652 ni shule za serikali.

“Na leo tunashuhudia mkoa ukiongeza shule moja ya kuifanya serikali kuwa na shule 653,” amesema.

Amesema idadi ya shule zinazofundisha kwa kutumia mtaala wa kiingereza mkoani Geita zipo 51 nyingine ni hiyo ya Museveni inafanya idadi kuwa 52.

“Kati ya hizo mbili zinamilikiwa na serikali, moja ipo halmashauri ya Geita na hii iliyopo Chato,” Mkuu wa Mkoa Geita.

“Katika wilaya ya Chato kuna shule za msingi 143, ikiwamo hii ya Museveni ambayo sasa itakuwa shule ya kwanza inayomilikiwa na serikali yenye mtaala wa kiingereza,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

NCCR-mageuzi yawaangukia Polisi kupotea kwa kada wake

Spread the loveJESHI la Polisi nchini limeombwa kufanya uchunguzi wa kina utakaosaidia...

Habari za Siasa

Uamuzi kesi ya kupinga Bodi ya Wadhamini NCCR-Mageuzi kutolewa Februari 6

Spread the love  MAHAKAMA Kuu, Masjala Kuu ya Dar es Salaam, imepanga...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu:Suluhu ya ugumu wa maisha ni Katiba Mpya

Spread the love  MAKAMU mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-Chadema Bara,...

Habari za Siasa

Lissu: Miaka 30 ya vyama vingi haikupambwa kwa marumaru

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-Chadema, Tundu...

error: Content is protected !!