January 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rangnick mwalimu wa Klopp, Tuchel ashushwa Manchester United

Spread the love

 

KLABU ya Manchester United imemtangaza Ralf Rangnick kuwa kocha mkuu wa muda wa klabu hiyo mara baada ya kumtimua Ole gunnar solskjaer kufuatia timu hiyo kupata matokeo mabovu. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Rangnick mwenye umri wa miaka 63, raia wa Ujerumani ameingia mkataba mpaka mwisho wa msimu wa 2021/22, huku kukiwa na kipengere cha kuongeza.

Kocha huyo ambaye ametajwa na vyombo vingi vya habari hivi karibuni kama mrithi wa Solskjaer ndani ya viunga hivyo vya Old Trafford amekuwa akisifika kama miongoni mwa makocha bora ambao walivutia wengi.

Moja ya makocha sa sasa ambao wamepita kwenye mikono yake ni kocha wa klabu ya Liverpool Jurgen Klopp sambamba na Thomas Tuchel anaekinoa kikosi cha Chelsea.

Sifa moja ya kocha huyo mpya wa Manchester United ni kucheza mpira wa kushambulia kwa Spidi (Gegenpressing) katika dakika zote 90 za mchezo.

Kibarua cha kwanza cha kocha huyo ndani ya kikosi cha Manchester United, kitakuwa kwenye mchezo unafuata wa Ligi Kuu England dhidi ya Arsenal ambao utapigwa siku ya Alhamis, tarehe 2, Disemba, 2021, kwenye dimba la Old Trafford

error: Content is protected !!