Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia awataka viongozi Afrika kushirikiana mapambano ya rushwa
Habari za Siasa

Rais Samia awataka viongozi Afrika kushirikiana mapambano ya rushwa

Rais Samia Suluhu Hassan
Spread the love

RAIS wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema moja ya vikwazo vikubwa vya maendeleo barani Afrika ni pamoja na janga la rushwa ambalo linadhoofisha mifumo ya kitaasisi na kuathiri mipango na mikakati ya kujikomboa kiuchumi. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Rais Samia Suluhu Hassan akipokea Tuzo kutoka Bodi ya Ushauri ya Kupambana na Rushwa Afrika iliyowasilishwa na Makamu Mwenyekiti wa AUABC, Pascoal Antonio Joaquim.

Rais Samia amesema hayo leo tarehe 11 Julai 2023 wakati wa kilele cha maadhimisho ya Siku ya Mapambano dhidi ya Rushwa Barani Afrika na maadhimisho ya utekelezaji wa miaka 20 ya Mkataba wa Umoja wa Afrika wa Kuzuia na Kupambana na Rushwa yaliyofanyika AICC.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akinyanyua juu tuzo kutoka Bodi ya Ushauri ya Kupambana na Rushwa Afrika mara baada ya kukabidhiwa wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya mapambano dhidi ya rushwa Barani Afrika yaliyofanyika katika ukumbi wa Nyasa uliopo kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa AICC Jijini Arusha tarehe 11 Julai, 2023.

Aidha, Rais Samia amesema viongozi wote barani Afrika hawana budi kuimarisha ushirikiano katika mapambano dhidi ya rushwa.

Vile vile, Rais Samia amewataka viongozi kutafakari na kuchambua kwa dhati masuala ya rushwa ili kubainisha changamoto au vikwazo vya mapambano hayo na kuchukua hatua muafaka.

Kwa upande mwingine, Rais Samia amesema Serikali inaendelea kuimarisha Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kibajeti na kimfumo ikiwemo

kuanzisha taasisi zinazosimamia utawala bora na haki za binadamu nchini.

Rais Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Kamishna wa Polisi (CP) Salum Hamduni kuhusu kazi mbalimbali ambazo Taasisi hiyo inafanya kwenye Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mapambano dhidi ya Rushwa Barani Afrika

Rais Samia pia amesema Serikali imewekeza zaidi katika matumizi ya mifumo ya TEHAMA inayosaidia kupunguza mawasiliano ya ana kwa ana katika kutoa huduma kama michakato ya zabuni, usajili wa biashara na namba ya mlipa kodi ili kupunguza mianya ya rushwa.

Amesema kupitia Divisheni ya Mahakama Kuu inayosikiliza kesi za washtakiwa wa makosa ya rushwa kubwa, Serikali imeokoa na kudhibiti matumizi ya fedha yasiyostahili ya zaidi ya Sh 139 bilioni kuanzia mwaka wa fedha 2019/20 hadi 2021/22.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kwafukuta kisa chaguzi, Lissu aibua tuhuma nzito

Spread the loveCHAGUZI za kusaka viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

error: Content is protected !!