Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Rais Mwinyi anusa ufisadi Bil. 9.65, amng’oa kigogo wa mapato
Habari Mchanganyiko

Rais Mwinyi anusa ufisadi Bil. 9.65, amng’oa kigogo wa mapato

Dk. HUssein Mwinyi, Rais wa Zanzibar
Spread the love

 

RAIS wa Zanzibar, Dk. Hussein Mwinyi, ametengua uteuzi wa Kamisha Mkuu wa Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB), Salum Yussuf Ali na kumsimamisha kazi Mkurugenzi wa Usajili, Ukaguzi na Upelelezi wa Walipa Kodi wa mamlaka hiyo, Hashim Kombo Haji, ili kupisha uchunguzi wa upotevu wa Sh. 9.65 bilioni. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar…(endelea).

Rais Mwinyi amechukua hatua hiyo leo Alhamisi, tarehe 17 Februari 2022, akizungumza na Bodi ya Wakurugenzi na Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumi Uchumi Zanzibar (ZAECA), katika ofisi za ZRB, visiwani Zanzibar.

Amesema, upotevu wa fedha huo umebainika baada ya uchunguzi kufanyika katika moja ya kampuni inayosafirisha abiria kwa meli.

“Kuna uchunguzi umefanywa wa moja ya makampuni yanayosafirisha abiria kwa meli, taarifa ya malipo yaliyooneshwa ya ulipaji na taarifa za uchunguzi kunaonyesha kuna utofauti wa ulipaji wa Sh.9 bilioni. Hazikulipwa ikaonekana kwamba mhusika kalipa mfumo umechezewa fedha hazikuonekana zilikokwenda,” amesema Rais Mwinyi.

Rais Mwinyi amesema, uchunguzi umebainisha kwamba, Haji aliamuru ripoti ya fedha hizo iondolewe isipelekwe kwenye uongozi, kisha Ali akaamuru ripoti ya uchunguzi huo isipelekwe katika bodi ya ZRB.

“Taarifa hiyo imefanywa na vijana wa hapa wa uchunguzi, imeletwa hapa menejiment mnayo taarifa hiyo. Kilichotokea ni nini, kilichotokea mkurugenzi wa usjaili, ukaguzi na mpelelezi wa walipa kodi Haji aliamuri ripoti hiyo iondolewe isipelekwe kwenye menejimenti,” amesema Rais Mwinyi na kuongeza:

“Ripoti hiyo ikapelekwa kwenye menejimenti, kilichofuatwa ripoti haikupelekwa kwenye bodi, kwa kibali cha kamishna mkuu ikaondolewa haikupelekwa kwenye bodi. Kwa hiyo bodi mnaweza mkawa hamjui lakini kipo hicho kitu.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!