Friday , 19 April 2024
Home Kitengo Maisha Elimu Serikali kujenga madarasa 12,000 mwaka 2022/2023
Elimu

Serikali kujenga madarasa 12,000 mwaka 2022/2023

David Silinde, Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)
Spread the love

 

Serikali kupitia mradi wa BOOST utakaotekelezwa katika Shule za Msingi inatarajiwa kujenga madarasa 12,000 katika mwaka wa fedha 2022/2023. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea)

Pia imesema itaendelea kutumia fedha za Mapato ya Ndani ya Halmashauri kujenga na kukarabati Shule za Msingi Kongwe.

Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 17 Februari, 2022 bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa nchi, ofisi ya Rais TAMISEMI, David Silinde wakati akijibu swali la Mbunge wa Newala Vijijini, Maimuna Salum Mtanda (CCM).

Mbunge huyo amehoji, je ni lini Serikali itaanza ukarabati wa Shule za Msingi Kongwe ambazo zimechakaa na majengo yake ni mafupi ulikinganisha na yanayojengwa kwa sasa.

Aidha, akijibu swali hilo Silinde amesema Serikali inatambua uwepo wa shule kongwe za msingi zilizo katika hali ya uchakavu na kazi ya kuzikarabati shule hizo ilishaanza kupitia miradi mbalimbali ya elimu.

Amesema Serikali inaendelea kuboresha miundombinu ya Elimu kwa kujenga na kukarabati miundombinu mbalimbali ya Shule za Msingi nchini.

“Katika mwaka wa fedha 2021/22 Serikali kupitia Programu ya EP4R (lipa kulingana na Matokeo) imeendelea na ujenzi wa vyumba vya madarasa ya shule za msingi 1,970, matundu ya vyoo 5,303, nyumba za walimu wa msingi 17, ujenzi huu ni kwa ajili ya kuboresha mazingira ya miundombinu ya shule za Msingi zikiwemo shule Kongwe ambazo zinamiundombinu chakavu.

“Vilevile kupitia Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Ta ifa na Mapambano dhidi ya UVIKO – 19 (TCRP), Serikali imejenga vyumba 3,000 vya madarasa katika vituo shikizi 970,” amesema na kuongeza kuwa;

“Serikali kupitia mradi wa BOOST utakaotekelezwa katika Shule za Msingi inatarajiwa kujenga madarasa 12,000 katika mwaka wa fedha 2022/2023 na itaendelea kutumia fedha za Mapato ya Ndani ya Halmashauri kujenga na kukarabati Shule za Msingi Kongwe.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuHabari za Siasa

Walimu 52,551 kupandishwa madaraja mwaka huu

Spread the loveNaibu Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala...

BiasharaElimu

NMB yatoa vifaa vya ujenzi kwa shule sita Nyasa  

Spread the loveBENKI ya NMB imetoa msaada wa vifaa mbalimbali vya ujenzi...

ElimuHabari Mchanganyiko

GGML yawapa mbinu wanafunzi Geita Boys kufikia malengo ya kitaaluma

Spread the loveKampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imetoa mafunzo maalumu...

ElimuHabari Mchanganyiko

Wanawake GGML wawanoa wanafunzi Kalangalala Sec. kujitambua

Spread the loveKATIKA kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani, Umoja wa...

error: Content is protected !!