Thursday , 2 February 2023
Home Gazeti Habari Rais Samia afunguka kesi ya Mbowe “tuiachie mahakama”
HabariTangulizi

Rais Samia afunguka kesi ya Mbowe “tuiachie mahakama”

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema akiingia mahakamani
Spread the love

 

KWA mara nyingine tena, Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amewataka watu wanaokosoa hatua ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kufunguliwa mashtaka ya ugaidi, kuiachia mahakama iamue kama ana kosa au hana kosa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Rais Samia ametoa kauli hiyo katika mahojiano yake na Idhaa ya Kiswahili ya Ujerumani (D.W Swahili), yaliyofanyika jijini Brussels nchini Ubelgiji, kurushwa katika mtandao wa idhaa hiyo leo Alhamisi, tarehe 17 Februari 2022.

Ni baada ya mtangazaji wa D.W Swahili, Sudi Mnette, kumuomba atoe ufafanuzi juu ya kauli yake aliyowahi kuitoa dhidi ya kesi ya uhujumu uchumi, namba 16/2021, inayomkabili Mbowe na wenzake katika Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, jijini Dar es Salaam.

“Nitatolea ufafanuzi kauli ngapi? Watu wanasema kila kauli kuhusu Rais, utazitolea zote ufaanuzi? Anayesema mwache aseme na nilisema mapema kwamba, mimi naruhsu freedom of speech (uhuru wa kuongea), sababu watu wakisema napata kujua wanayoyasema na mimi najua ya kuyarekebisha jinsi ninavyoendesha Serikali yangu,” amesema Rais Samia.

Rais Samia Suluhu Hassan

Rais Samia amesema “kwa hiyo kama wamesema, kila wanalosema nitalitolea ufafanuzi? Acha waseme tuiachie mahakama, kesi iko mahakamani mahakama itaamua ana kosa au hana kosa. Sisi hatuwezi kusema chochote.”

Agosti 2021, akihojiwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC Swahili), Rais Samia aliwataka wanaopiga kelele kuhusu kesi hiyo, waiachie mahakama kwani ndiyo itakayoamua kama ana hatia au hana hatia.

Katika kesi hiyo yenye mashtaka sita ya ugaidi, mbali na Mbowe, washtakiwa wengine ni waliokuwa makomando wa Jeshi la Ulinzi wa Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Halfan Bwire Hassan, Adam Kasekwa na Mohammed Abdillah Ling’wenya.

Kesi hiyo inasikilizwa mfululizo mbele ya Jaji Joachim Tiganga, ambapo kesho Ijumaa, mahakama hiyo inatarajia kutoa uamuzi mdogo kama wana kesi ya kujibu au hawana, baada ya upande wa mashtaka kufunga ushahidi.

Rais Samia Suluhu Hassan, akihojiwa na Idhaa ya Kiswahili ya Ujerumani (D.W Swahili), ameizungumzia kesi ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake, akisema “acha waseme tuiachie mahakama itaamua ana kosa au hana kosa, sisi hatuwezi kusema chochote.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Mo Dewji achomoza bilionea pekee Afrika Mashariki

Spread the loveMAZINGIRA mazuri ya uwekezaji nchini Tanzania yamezidi kuleta matunda baada...

Habari MchanganyikoTangulizi

Bilioni 213 za miradi ya DMDP zaistawisha Temeke

Spread the loveJUMLA ya Sh bilioni 213 zimetumika kuboresha sekta ya afya,...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Bashiru aibuka na bei za vyakula, “Njaa inadhalilisha nchi”

Spread the loveMBUNGE wa kuteuliwa na Rais, Dk. Bashiru Ally, ameitaka Serikali...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ahoji fedha za Plea-Bargaining

Spread the love  RAIS Samia Suluhu Hassan, ameitaka Tume ya kuangalia namna...

error: Content is protected !!