May 8, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Rais Magufuli ametufanya tutembee kifua mbele – Zitto

Spread the love

MBUNGE wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), amesema kuwa hatua ya Rais John Magufuli, kuzuia matumizi ya kanuni mpya za vikokotoo kwa ajili ya wafanyakazi waliostaafu, ni ishara tosha ya umakini wa hoja za kambi ya upinzani. Anaripoti Yusuph Katimba … (endelea).

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, aliyoitoa muda mfupi baada ya Rais Magufuli kumaliza kuzungumza na vyama vya wafanyakazi, Zitto anasema, uamuzi wa rais juu ya “vikokotoo,” umewaumbua baadhi ya mawaziri na kuuwinua upinzani.

Zitto ambaye ni kiongozi mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo anasema, “uamuzi wa rais kuhusu kikokotoo cha mafao ya pensheni kwa wastaafu, sisi ACT Wazalendo na vyama vya upinzani kwa ujumla, tumesimama na wafanyakazi toka mwanzo wa sakata hili.”

Anasema, tokea mwanzo ambako sheria ilikuwa muswada na hata baada ya kanuni kutungwa, bado wao walibaki na wafanyakazi na kuwatetea kwa gharama zote.

Anasema, “kwetu, jambo lolote linaloongeza maslahi na ustawi wa wafanyakazi ni jambo jema na muhimu. Tunashukuru kuwa mheshimiwa Rais ametuelewa na amekuja upande wetu na kuacha upande wa waziri wake, washauri wake na watendaji wa serikali yake.”

Mwanasiasa huyo machachari nchini anaonya kuwa …“kwetu, huu si wakati wa kunyang’anyana sifa. Washindi ni wafanyakazi na Watanzania.”

Zitto anaeleza katika taarifa yake kuwa “tunapoelekea mbele, tunamuomba asiwe na aibu kutusikiliza na mengine mengi kwa kuwa nia yetu ni njema tunajenga nchi moja.

“Atusikilize na kuhusu mishahara ya watumishi wa umma, atusikilize kuhusu mateso ya wakulima wa korosho na atusikilize kuhusu sheria ya vyama vya siasa. Kama hili la wafanyakazi hatukutumwa na mabeberu, basi na mengine pia hatutumwi na mabeberu.”

error: Content is protected !!